Sunday, December 2, 2012

TANZANIA TUJIFUNZE TOKA KENYA


Serikali ya Kenya imeanza kutekeleza sheria mpya ya kuzuia madereva wanatakaoendesha magari katika hali ya hatari, Sheria ambayo imeanza kutekelezwa tangu Jumamosi.
Mwanamke akata bara-bara nchini Kenya
Kwa upande wao madereva wa mabasi ya abiria nchini humo maarufu kama matatu, wamekuwa wakigoma tangu Alhamisi mjini Nairobi na kwengineko, kulalamika juu ya sheria hiyo.
Kwa mujibu wa sheria hiyo mpya iliyoanzishwa kwa dereva yeyote atakayekutwa na kosa atapewa adhabu kali pamoja na kifungo cha maisha. Wengi wanasema kuwa hawamudu faini kubwa. 
Kwa hili serikali imeazimia kupunguza vifo mabara-barani. Mwaka uliopita Wakenya zaidi ya 3,000 wamekufa kwenye ajali za barabarani.
Serikali ya Tanzania imelipata hili?

No comments:

Post a Comment