Thursday, November 15, 2012

WATANZANIA, JE WAPO TAYARI KWENDA KATIKA MFUMO WA DIGITALI?

Watanzania wametakiwa kujiandaa kukabiliana na mabadiliko ya tecknolojia kuachana na analojia na kuhamia kwenye digitali yanayotarajiwa kuanza tarehe 31 ya mwenzi wa kumi na mbili mwaka huu.

Hayo yamesemwa na waziri wa sayansi na tecknolojia Prof. Makame Mbarau alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kutaka kujua hatua za mwisho za kuachana na analojia na kuhamia katika mfumo digitali.


Na Robert latonga
Ikiwa Tanzania ipo sambamba katika mabadiliko ya Sayansi na tecknolojia kama nchi  nyingine zilizoendelea duniani ni takribani mwezi mmoja na nusu umebaki Tanzania kuachana na mfumo wa zamani wa analojia na kuhamia mfumo mpya wa digitali lakini swali la kujiuliza ni kwamba je watanzania wako tayari kukabiliana na mabadiliko hayo.

Mheshimiwa Mbarawa anasisitiza kuwa ni vyema wananchi wakajiandaa kukabiliana na mfumo huu hasa katika muda huu mchache uliobaki katika kukabiliana na mabadiliko ya sayansi na tecknolojia kwa kuanza kutumia digital
Mmoja wa wadau wa mabadiliko ya urushaji wa matangazo ya televisheni kutoka katika mfumo wa analojia kwenda Digitali Bw. Isa Mbura akiwasilisha mawazo yake juu ya nini kifanyike ili kuboresha urushaji wa matangazo hayo pindi tu yatakapoanza mnamo tar 31/12/2012
Lakini licha ya jitihada za serikali kupitia mamlaka ya mawasiliano Tanzania kujitahidi kuwaabarisha wananchi dhidi ya mabadiliko ya analogy kuhamia digital lakini bado katika jiji la dar es salaam  kuna changamoto kubwa hasa kwa wananchi wa kada chini wasiojua mabadiliko haya

Makubaliano ya nchi zote duniani ni kuhakikisha ifikapo mwaka elfu mbili na kumi na tano ziwe katika mfumo mmoja wa digitali na kuachana na mfumo wa zamani wa analojia, na kwa Tanzania mabadiliko hayo yanatakiwa kuanza rasmi tarehe 31/12/2012

No comments:

Post a Comment