Wednesday, October 24, 2012

WASOMI VYUO VIKUU: ''VYOMBO VYA HABARI VIIHAMASISHE JAMII KUACHANA NA RUSHWA''

VYOMBO vya habari vimepewa jukumu la kuelimisha kutaarifu na kuhamasisha Umma katika masuala mbalimbali yaliyopo katika jamii.

Kwa kuyatambua hayo mwandishi wa mtandao huu anapata fursa ya kuzungumza na Mhadhiri Msaidizi wa chuo Kikuu cha Tumaini - Iringa bw. Simon Berege ambaye anazungumzia ni jinsi vyombo vya habari vina wajibu wa kupambana na rushwa.

Anaanza kwa kusema;
''Tunategemea kwamba vyombo vya habari vifanye kazi zaidi, vivuke mipaka ya kuhabarisha, kuburudisha, kushawishi na hatimaye vijikite katika majuku maalum, ambayo ni kupambana na rushwa kwaajili ya maslahi ya taifa''

Bw. Simon akaenda mbali zaidi kwa kuongelea suala  ushawishi wa vyombo vya habari kuwa ni mkubwa sana katika jamii, hivyo vyombo vya habari havinabudi kuishawishi jamii kuepukana na masuala mazima ya vitendo vya rushwa.

Bw. Simon Berege, Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Tumaini - Iringa akiongea na mwandishi wa habari kuhusiana na masuala ya rushwa.
kabla ya kuondoka katika eneo hilo mwandishi wa mtandao huu anapata fursa pia ya kuzungumza na Agnes Shija ambae ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu - Tumaini cha Dar es salaam, nae anaeleza umuhimu wa kukemea rushwa kupitia vyombo vya habari.

''Hali ya vyombo vya habari kwa sasa katika mchakato mzima wa kupambana na rushwa kwakweli ni wa kiwango cha juu, kwasababu vyombo hivyo vimejitahidi kufichua kila matendo ya rushwa yanapotokea lakini pia vimeonesha hasara zinazojitokeza pale ambapo matukio hayo yanapojitokeza kwa mfano masuala ya EPA, ubadhilifu wa ardhi n.k kitu ambacho kimewawezesha wananchi kufahamu hali halisi na chanzo cha matatizo yao, lakini pia kuwaonesha njia kuwa wanahaki ya kufuatilia kisheria na kuyapeleka matatizo yao katika sehemu husika zinazoshughulikia masuala ya rushwa'' alisema Bi. Agnes Shija.
Bi. Agnes Shija, Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Tumaini - Dar es salaam akiongea na mwandishi wetu juu ya umuhimu wa vyombo vya habari kupambana na rushwa katika jamii. 


Rushwa bado imekuwa kikwazo katika nchi zinazoendelea, hivyo hatuna budi kama wanajamii kuungana kwa pamoja mimi, wewe na yule kuipinga na kupingana kabisa na vitendo vya utoaji na upokeaji rushwa ya aina yeyote ile; hapa nikimaanisha rushwa ya ngono, fedha mali n.k

Kwa nguvu moja wananchi tuipinge RUSHWA!
k

No comments:

Post a Comment