Monday, October 29, 2012

USAFIRI WA RELI WAANZA DAR

Wananchi wafurahia  Dkt. Mwakyembe awa abiria wa kwanza


Ni kwa muda mrefu sasa sakata la foleni jijini Dar limekuwa likiwakera wengi kutokana na kukaa barabarani kwa muda mrefu na kusababisha mzunguko wa fedha kuwa mdogo, jambo ambalo limekuwa likiongeza ugumu wa maisha kila kukicha.
Mara nyingi wakazi wa Mba... hukumbwa na kadhia hii. kwa usafiri huu wa tren ni uhakika wetu kuwa mambo yatakua safi.


Picha tofauti zikionyesha magari yakiwa katika foleni jijini Dar es salaam

Serikali kwa kulitambua tatizo kama linavyoonekana hapo juu, kupitia wizara ya uchukuzi imezindua usafiri wa treni kutokea ubungo mpaka katikati ya jiji la dar es salaam.
Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harison Mwakyembe akizindua huduma ya Usafiri wa treni katika jiji la Dar es salaam, Kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa TAZARA Damas Ndumbaro.
Dkt. Mwakyembe anapata fursa ya kuzindua usafiri huo ambao ulijumuisha na ule unaotokea TAZARA mpaka mwakanga nje kidogo ya jiji la Dar es saalam 
Watanzania wengi wameupokea vizuri usafiri huo wa treni ambao kwa muda mrefu umekuwa ukitumiwa kwa safari za mikoani pamoja na nje ya mipaka ya Tanzania.

''Tunashukuru kwa kuwekewa usafiri huu wa treni kwani tunauhakika utapunguza msongamano wa barabarani, tunaamini kwa huduma kama hizi za haraka shughuli zetu zitaenda kwa haraka, kwani usafiri wa daladala unaweza ukakaa kituoni kwa mda mrefu'', alisema mmoja wa wananchi aliehudhuria katika uzinduzi huo.

Jitihada za serikali ya nne, zikiongozwa na Dkt. Jakaya Kikwete pamoja na waziri wa uchukuzi Dkt. Harison Mwakyembe wanapiga hatua moja mbele kwa kufanikisha usafiri huu wa treni ili kupunguza kero ya foreni jijini iliyokuwa kikwazo cha maendeleo.

Dkt. Mwakyembe akapaza sauti yake kwa kusema kuwa anajivunia moja kati ya mikakati iliyotolewa na serikali ya chama cha mapinduzi CCM.
Dkt. Mwakyembe akihutubia katika uzinduzi wa usafiri wa treni ambao utakuwa unafanywa kutoka katikati ya hadi nje kidogo ya jiji.
''Tukizingatia kwamba ilani ya uchaguzi ya CCM  pamoja na kauli za viongozi wetu wandamizi wa nchi zinataka uborreshaji wa huduma za usafirishaji katika majiji yetu, tukasema ngoja tuwaombe hawahawa mafundi wetuwatafute vichwa vya treni, injini ambazo ni mbovu, mabehewa yaliyochakaa ili tuyafufue upya, wengi walidhani ni ndoto lakini naomba niwapongeze mafundi wetu wafanyakazi wa karakana yetu ya TAZARA Dar es salaam ambayo wameifanya'' alisema Mwakyembe.


Dkt. Mwakyembe pia amewaasa wakazi wa jiji la Dar es salaam kufuata utaratibu uliowekwa ikiwa ni pamoja na kukata tiketi wakati wa safari na ambapo akata nauli kuwa ni Tsh. 400 kwa watu wazima na Sh. 100 kwa wanafunzi.


Pia mwandishi wa mtandao huu wa ulimwenguwahabari.blogspot.com alipata fursa ya kuongea na Dkt. Mwakyembe kuhusu usafiri wa majini ulioahidiwa na serikali unaotoka kivukoni mpaka bagamoyo ili kupunguza kero ya foreni jijini.
Akasema ''tunaangalia wenzetu wa wizara ya ujenzi ambao wameliongelea hilo suala wamefikia wapi kisha kama tutaona kama kuna kukwama tutaongezea juhudi nasi tumejipanga kuwa mwaka ujao tuweze kuanzisha huduma ya meli baharini'' 

No comments:

Post a Comment