Polisi wa kutuliza ghasia (FFU) wakifanya doria, kuzunguka eneo la kariakoo, wakihakikisha ulinzi unaimarika. |
Ni gari la jeshi la JWTZ lililokuwa limewabeba wanajeshi, likirandaranda huku na kule katika eneo la kariakoo, likihakikisha kuwa amani inarejea maeneo hayo. |
Polisi wa kutuliza ghasia (FFU) wakitoa onyo kwa wananchi waliokuwa wamekusanyika katika maeneo hayo, waondoke haraka. |
Kikosi cha JWTZ kikiwa kazini. (Picha zote kwa Hisani ya Kishindoleo.blogspot.com) |
CHANZO!
Chanzo cha vurugu hizo ni watoto wawili wa dini tofauti ( mmoja kutoka dini ya kiislamu na mwingine dini ya kikristo) walipokuwa wanagombana na hatimaye mtoto wa kikristo kufikia hatua ya kukojolea Msaafu jambo ambalo lilizua vurugu kubwa na kusababisha mali kuvunjwa pamoja na makanisa kuchomwa moto.kutokana na vurugu hizo zilizotokea leo, zilipelekea shughuli mbalimbali katika eneo kusitishwa ikiwa ni pamoja na maduka kufungwa.
Polisi wa kutuliza ghasia, migambo pamoja na JWTZ walitanda kila eneo kuhakikisha amani inarejea eneo hilo.
Mpaka mwandishi wa habari wa mtandao huu wa www.ulimwenguwahabari.blogspot.com anarejea mtamboni iliripotiwa kuwa pikipiki moja ilikuwa imeharibiwa vibaya.
No comments:
Post a Comment