Wednesday, October 31, 2012

TFDA YATOA UFAFANUZI JUU YA DAWA BANDIA ZA ARVs


Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Mr. Hiiti Sillo akiwaonesha waandishi wa habari fomu ya kukusanyia madhara ya dawa.

1.0        UTANGULIZI

a).    Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ni Wakala wa Serikali chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii yenye jukumu la kudhibiti usalama, ubora na ufanisi wa chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba ili kulinda afya ya jamii. TFDA imeweka mifumo mbalimbali ya udhibiti chini ya sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi, Sura 219. Mifumo hiyo ni pamoja na usajili wa bidhaa, usajili wa majengo/maeneo ya kuzalisha na kuuza bidhaa, uchunguzi wa kimaabara wa sampuli za bidhaa pamoja na ukaguzi na ufuatiliaji wake kwenye soko.

b).    Kupitia mifumo iliyowekwa, TFDA imekuwa ikihakikisha usalama, ubora na ufanisi wa dawa katika soko. Aidha, mifumo hiyo pia huwezesha kubaini uwepo wa bidhaa bandia na duni kwenye soko na kuchukua hatua mbalimbali kwa mujibu wa Sheria. Hatua hizo ni pamoja na kusitisha matumizi ya bidhaa husika na kuziondoa kwenye soko, kuziteketeza na kuwafikisha watuhumiwa kwenye vyombo vya dola na sheria.

c).  Itakumbukwa kwamba, mnamo tarehe 21 Septemba 2012, tarehe 4 Oktoba, 2012 na tarehe 10 Oktoba 2012,  Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii  ilitoa taarifa kwa umma juu ya uwepo wa dawa bandia ya kupunguza makali ya UKIMWI yenye jina la kibiashara ‘TT-VIR 30’ toleo Na. 0C.01.85 ikiwa ni pamoja na hatua zilizochukuliwa. Baada ya taarifa hizi za Wizara kutolewa, kumekuwa na taarifa mbalimbali kupitia vyombo vya habari zinazoleta mkanganyiko kwa wananchi kuhusu suala hili.

d). Baadhi ya mikanganyiko hiyo ni pamoja na jinsi dawa hiyo bandia ilivyobainika, kama barua za TFDA ziliwafikia Tanzania Pharmaceuticals Industries (TPI) Ltd na kama uzalishaji wa dawa bado unaendelea au la.

e).    Ili kuondoa mkanganyiko ambao umeanza kujitokeza, Mamlaka inapenda kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu dawa hizo bandia ambazo matumizi yake yamesitishwa. Vilevile,  TFDA inapenda kutumia fursa hii kutoa ufafanuzi kuhusu mfumo wa udhibiti wa dawa nchini.

2.0     UFAFANUZI KUHUSU DAWA BANDIA YA TT-VIR 30
  • TFDA ndiyo iliyobaini uwepo wa dawa bandia aina ya TT-VIR 30 toleo Na. 0C.01.85 kwenye soko mnamo tarehe 28 Julai, 2012 kupitia mfumo wake wa ukaguzi na ufuatiliaji wa bidhaa katika soko. 
  • Kama ilivyoelezwa katika taarifa zilizotolewa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, TFDA inasisitiza kwamba kampuni ya TPI Ltd iliiuzia MSD dawa bandia aina ya TT-VIR 30 toleo Na. 0C.01.85, kwa mujibu wa nyaraka zilizopo.
  • Nyaraka hizo pamoja na vielelezo mbalimbali zimewasilishwa kwenye vyombo vya usalama kwa hatua zaidi za kisheria.
  • TFDA imesitisha uzalishaji wa dawa za ARVs za kiwanda cha TPI Ltd kupitia barua Kumb. Na. CA/C.80/222/01A/47 ya tarehe 4 Oktoba, 2012 na vile vile uzalishaji na usambazaji wa dawa zote kupitia barua Kumb. Na. CA/C.80/222/01A/55 ya tarehe 10 Oktoba, 2012.
  • Barua hizo zilipelekwa kwa ‘dispatch’ katika ofisi za Makao Makuu ya Kampuni ya TPI Ltd iliyoko eneo la Mikocheni, Dar es Salaam na kupokelewa tarehe 04 na 10 Oktoba, 2012.
  • Taarifa zilizotolewa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii zilionesha wazi kwamba TFDA ndiyo iliyositisha uzalishaji wa dawa katika kiwanda cha TPI Ltd.
  • Ukaguzi uliofanywa na TFDA kwenye kiwanda cha TPI Ltd, Arusha tarehe 12 na 23 Oktoba 2012, umethibitisha kwamba hakuna uzalishaji wa dawa unaoendelea kwenye kiwanda husika kama ilivyoelekezwa na TFDA.
3.0        MFUMO WA UDHIBITI WA DAWA NCHINI

Aidha, Mamlaka inapenda kutumia fursa hii kufafanua zaidi kuhusu mfumo wa udhibiti wa dawa nchini kama ifuatavyo;

a).    Udhibiti wa dawa unazingatia Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi, Sura 219, kanuni zilizowekwa, miongozo, misingi ya kisayansi (science based) pamoja na miundombinu kama vile maabara na mtandao wa ukaguzi. Mifumo ya udhibiti hujumuisha yafuatayo;-
                             i.        Kufanya tathmini ya taarifa za kisayansi kuhusu ubora, usalama na ufanisi wa dawa, kufanya ukaguzi wa viwanda na hatimaye kusajili dawa husika.
                           ii.        Kusajili maeneo yanayojishughulisha na uzalishaji na biashara ya dawa ikiwepo masharti ya kuwa na wataalam wa kusimamia uzalishaji.
                          iii.        Kufanya ukaguzi wa maeneo yanayotengeneza dawa, vituo vya forodha pamona na maeneo ya kusambaza na kuuza dawa.
                          iv.        Kufanya ufuatiliaji wa ubora, usalama na ufanisi wa dawa zilizosajiliwa kwa lengo la kuhakikisha kwamba zinakidhi vigezo na matakwa ya usajili.
                            v.        Kufanya uchunguzi wa kimaabara ili kuhakiki usalama na ubora wa dawa zinazoombewa usajili na zile zilizoruhusiwa kutumika nchini.

b).    Katika kutekeleza mifumo ya udhibiti na kwa kuzingatia misingi ya udhibiti wa bidhaa duniani, mwenye jukumu la kwanza la kuhakikisha usalama, ubora na ufanisi wa bidhaa ni la aliyeisajili bidhaa (marketing authorization holder) ili kuhakikisha kuwa mtumiaji hapati madhara.

c).    Mifumo hii ndiyo inayoiwezesha TFDA kuhakikisha usalama, ubora na ufanisi wa dawa na pia kubaini dawa bandia na duni katika soko na kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria.

4.0        HITIMISHO

a).    Uchunguzi zaidi wa dawa bandia aina ya TT-VIR 30 toleo Na. 0C.01.85 unaendelea kupitia vyombo vya usalama kwa hatua zaidi za kisheria.

b).    TFDA itaendelea kufuatilia usalama, ubora na ufanisi wa dawa kwenye soko kupitia mifumo iliyowekwa ili kulinda na kudumisha afya ya jamii;

c).    Tunapenda kuwakumbusha wote wanaojihusisha na biashara ya dawa, chakula, vipodozi na vifaa tiba kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo iliyowekwa na kwamba yeyote atakayekiuka taratibu hizo atachukuliwa hatua kali za kisheria.

d).    Tunawahakikishia wananchi kwamba dawa za ARVs zilizoko katika vituo vya kutolea huduma za afya ni salama na hivyo waendelee kuzitumia bila wasiwasi wowote.

e).    Tunatoa rai kwa vyombo vya habari, watoa huduma za afya na wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa pale wanapobaini au kuhisi kuwepo kwa chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba vyenye mashaka au uvunjifu wa Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi, Sura 219.

Hiiti B. Sillo
MKURUGENZI MKUU
MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA
30 OKTOBA, 2012

TUNAENDA SHULE JAMANI!

Kamera yetu Mtaani ilifanikiwa kupata picha ya Wanafunzi wa shule ya msingi Mkwalia Kitumbo wilaya ya Mkuranga Mkoani pwani wakilazimika kuvua viatu pindi wanapotaka kuvuka dimbwi la maji, wakiwa wanaelekea shuleni kwao. (Picha na Ochieng Gad Ogweno)

Monday, October 29, 2012

HONGERA DKT. AYOUB RIOBA


Dkt. Ayoub Rioba akihutubia muda mfupi baada ya kutunukiwa shahada ya udaktari wa falsafa (PHD) katika fani ya falsafa ya jamii chuo kikuu cha Tampere katika jiji la Tampere, Finland.
Hapa Dkt. Ayub Rioba (University of Dar es salaam - School of Journalism and Mass Communication) Kushoto, Prof Kaarle Nordenstreng (University of Tampere, Finland) Katikati, Prof. Audrey Gadzekpo (Accra University, Ghana) mwishoni kulia. Dkt. Rioba alikuwa akijibu maswali kutokana na utafiti wake wa 'Media Accountability in Tanzania's Multiparty democracy; Does self regulation work?'
Kutoka kushoto Prof Kaarle Nordenstreng, University of Tampere Finland  pamoja na Prof Audrey Gadzekpo akiongoza mchakato wa kumtunukia falsafa ya udaktari Ayub Rioba. (Picha zone na  PAULA PAUKKU)

USAFIRI WA RELI WAANZA DAR

Wananchi wafurahia  Dkt. Mwakyembe awa abiria wa kwanza


Ni kwa muda mrefu sasa sakata la foleni jijini Dar limekuwa likiwakera wengi kutokana na kukaa barabarani kwa muda mrefu na kusababisha mzunguko wa fedha kuwa mdogo, jambo ambalo limekuwa likiongeza ugumu wa maisha kila kukicha.
Mara nyingi wakazi wa Mba... hukumbwa na kadhia hii. kwa usafiri huu wa tren ni uhakika wetu kuwa mambo yatakua safi.


Picha tofauti zikionyesha magari yakiwa katika foleni jijini Dar es salaam

Serikali kwa kulitambua tatizo kama linavyoonekana hapo juu, kupitia wizara ya uchukuzi imezindua usafiri wa treni kutokea ubungo mpaka katikati ya jiji la dar es salaam.
Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harison Mwakyembe akizindua huduma ya Usafiri wa treni katika jiji la Dar es salaam, Kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa TAZARA Damas Ndumbaro.
Dkt. Mwakyembe anapata fursa ya kuzindua usafiri huo ambao ulijumuisha na ule unaotokea TAZARA mpaka mwakanga nje kidogo ya jiji la Dar es saalam 
Watanzania wengi wameupokea vizuri usafiri huo wa treni ambao kwa muda mrefu umekuwa ukitumiwa kwa safari za mikoani pamoja na nje ya mipaka ya Tanzania.

''Tunashukuru kwa kuwekewa usafiri huu wa treni kwani tunauhakika utapunguza msongamano wa barabarani, tunaamini kwa huduma kama hizi za haraka shughuli zetu zitaenda kwa haraka, kwani usafiri wa daladala unaweza ukakaa kituoni kwa mda mrefu'', alisema mmoja wa wananchi aliehudhuria katika uzinduzi huo.

Jitihada za serikali ya nne, zikiongozwa na Dkt. Jakaya Kikwete pamoja na waziri wa uchukuzi Dkt. Harison Mwakyembe wanapiga hatua moja mbele kwa kufanikisha usafiri huu wa treni ili kupunguza kero ya foreni jijini iliyokuwa kikwazo cha maendeleo.

Dkt. Mwakyembe akapaza sauti yake kwa kusema kuwa anajivunia moja kati ya mikakati iliyotolewa na serikali ya chama cha mapinduzi CCM.
Dkt. Mwakyembe akihutubia katika uzinduzi wa usafiri wa treni ambao utakuwa unafanywa kutoka katikati ya hadi nje kidogo ya jiji.
''Tukizingatia kwamba ilani ya uchaguzi ya CCM  pamoja na kauli za viongozi wetu wandamizi wa nchi zinataka uborreshaji wa huduma za usafirishaji katika majiji yetu, tukasema ngoja tuwaombe hawahawa mafundi wetuwatafute vichwa vya treni, injini ambazo ni mbovu, mabehewa yaliyochakaa ili tuyafufue upya, wengi walidhani ni ndoto lakini naomba niwapongeze mafundi wetu wafanyakazi wa karakana yetu ya TAZARA Dar es salaam ambayo wameifanya'' alisema Mwakyembe.


Dkt. Mwakyembe pia amewaasa wakazi wa jiji la Dar es salaam kufuata utaratibu uliowekwa ikiwa ni pamoja na kukata tiketi wakati wa safari na ambapo akata nauli kuwa ni Tsh. 400 kwa watu wazima na Sh. 100 kwa wanafunzi.


Pia mwandishi wa mtandao huu wa ulimwenguwahabari.blogspot.com alipata fursa ya kuongea na Dkt. Mwakyembe kuhusu usafiri wa majini ulioahidiwa na serikali unaotoka kivukoni mpaka bagamoyo ili kupunguza kero ya foreni jijini.
Akasema ''tunaangalia wenzetu wa wizara ya ujenzi ambao wameliongelea hilo suala wamefikia wapi kisha kama tutaona kama kuna kukwama tutaongezea juhudi nasi tumejipanga kuwa mwaka ujao tuweze kuanzisha huduma ya meli baharini'' 

POLISI DAR WAKAMATA NYARA ZA SERIKALI

Pembe za ndovu ziliokamatwa na Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam maeneo ya Kimara Jijini Dar.

Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam linawashikilia watuhumiwa watuhumiwa wanne wa nyara za serikali akiwemo mwanamke mmoja, raia wawili wa kenya kwa vitendo vya ujangili baada ya kukamatwa na meno ya tembo miambili na kumi na nne (214) zikiwa na thamani ya Tsh. Bilioni 2 milioni moja na 59 elfu laki moja na 57 kinyume cha sheria.

''Jeshi la polisi kanda maalumu lilipata taarifa kuwa huko kimara kwa mzee Kenyelaki kwamba kuna waarifu walikuwa mameficha mali mbalimbali ikiwa ni pamoja na nyara za serikali, tulipofika katika hiyo nyumba tukakuta wanaashi wakenya wawili pamoja na mtanzania mmoja ambae ni mwanamke, katika upekuzi wa nyumba hiyo vilipatikana vitu mbalimbali vilivyokuwa vimeibiwa kama mafriji, magoro na nyara.

Wakati huo huo pia kamanda Kova akatumia kupiga marufuku vikundi vinavyojihusisha kuwepo kwa tetesi za maandamano yanayotarajiwa kufanyika siku ya Alhamisi na Ijumaa kwa waumini wa dini ya kiislamu na kuwepo kwa vipeperushi vinavyoashiria uvunjifu wa amani.
''Suala hilo la maandamano halikubaliki saizi na hatuna mazungumzo zaidi katika suala lolote ambalo litaashiria uvunjifu wa aman, sisi hatuangalii dini, chama, taasisi au nani anasema, tunachoangalia ni Law and Order,(Sheria na utaratibu) Alisema Kova.

Mkuu wa kikosi cha kuzuia ujangiri 

Sunday, October 28, 2012

SJMC NIGHT ILIVYOKOSHA NYOYO ZA WENGI.

vvvvKufahamu mazingira yanayokuzunguka huwa ni jambo jema sana kwa binadamu kwani humpa mwanadamu kujiamini kwa kile anachokifanya katika mazingira aliyopo.

Kufahamiana na watu aliowakuta katika mazingira hayo mageni pia huleta faraja na amani kwani hupata kujua historia mbalimbali za eneo hilo; watu, viumbe au hata vitu ambavyo vimeshawahi kuishi katika eneo hilo, na vinavyoendelea kuishi.

Vilevile moja kati ya vitu muhimu duniani ambavyo binadamu anapaswa kuwa navyo ni pamoja na kupata muda wa kurefresh na kuanza upya, kwani hata kiafya hupunguza msongo wa mawazo na kurejesha hali mpya katika mfumo mzima wa ufahamu na kupelekea ufanisi kuongezeka na afya ya akili kuimarika.

Kwa kulitambua hilo Serikali ya wanafunzi DARUSO-SJMC iliona ni vyema kuaandaa  hafla fupi ya kuwakaribisha wanafunzi wa certificate na mwaka wa kwanza ambao wao ni wageni katika mazingira haya kujumuika na wenzao wanaoendelea (continuous) kufurahia ujio wao hapa chuo na kufurahia kukutana na vijana wenyeji wenye kuwapenda wageni wao.

Kulikuwa na matukio mengi ambayo kiukweli ukifuatilia katika mfululizo hapa chini utagundua kuwa tukio hili lilikuwa ni maalumu kwa freshers na wenyeji wao kula bata!!! KARIBU UJIONEE...
Hafla hiyo ilianzwa kwa wadau wote kushiriki katika michezo.
Haya sasa wenye. 1, 2, 3 twendeeeeeh!!!
Vutaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!! jamani wewe usiachieeee!!!!!!
Chezea sisi wewe!!! Sisi ndio washindi, Hureeeeeh!!!!!!!!!!!
Haya sasa nani kidume!!!! twendeee vutaaaaaaaaaa!!!!!!!!
Bravooooo!!! Sam Mwalongo, Riziki Mashaka, Denis, Yasin mpooooo!!!!!?
Ngoja tuingie ukumbini sasa!!!
Tumetokelezea eeeeeh!!!!!!!? 







Ndipo baada ya michezo hiyo kamati teule ya shughuli hiyo, ikatambulishwa!!!

Mgeni rasmi mkuu wa shule kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa  Umma (SJMC) Dkt. Herbert Makoye akiwa na M/kiti wa Serikali ya wanafunzi DARUSO-SJMC Bw. Musa Ngwegwe, wakitazama shughuli inavyokwenda.
Mgeni rasmi mkuu wa shule kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa  Umma (SJMC) Dkt. Herbert Makoye akitoa nasaha kwa wanafunzi wa SJMC pamoja na wageni waalikwa waliokuwapo ukumbini hapo.


Baadhi ya wanafunzi na wageni waalikwa wakiwa bize kushudia shoo ya vijana matata (katika picha inayofuata)

Ebwana eeeh!! hawa kinadada balaa, usiwaone ukadhani wazembe. kwenye mguu upande wako fiti kalikiti.

Hii ni ME COLLECTION: Mamodo wamepozi katika foto ya pamoja huku wakiwa wametinga nguo bomba kutoka ME COLLECTION inayosimamiwa na mwanadada Dorcas Francis

Warembo wakiwa wametokelezea, wakiongozwa na mama Nice Lucas Siema (alievaa nguo ya madoamadoa) wakichabo mpango mzima wa shoo pale Girrafe Ocean View Hotel!

Warembo wa mwaka wa kwanza wakiwa wametokelezea kwa sana!!! safi sana.

Kwa wageni waalikwa nao ilikuwa ni shangwe kwani waliyazoea mazingira fasta na kula 'monde' kama kawa


Boy: Hey ujue umependeza na mimi nimepe so kama vipi tutacheza wote mziki eeh!
Girl: Mmmh!!!





Anonymus: ''Oya nani anaelewa ratiba inayofuatia???


Menu ilikaa poa balaa


Wosia kidogo kutoka kwa baba, Mwalimu Isa Mbura it was great having you sir.

Mziki ukafunguliwa bwana, kilichoendelea nadhani unaona picha hapo chini.
Kitu na boksi!
Freestyle sasa! Mc BRAVO akishusha mambo!
  (Picha zote na Hilali Ruhundwa 'PHD')