Sunday, September 20, 2015

DIAMOND PLATNUMZ AMWANIKA MWANAE TIFFAH, NMB WASIMAMIA SHOO *PICHAZ*

“Huyu Ndio Binti yangu…Latiffah Binti Nasibu Abdul almaaruf kama @Princess_tiffah… Kila mmoja wetu anaweza kumfungulia mwanae NMB Junio Accont na kumuifadhia fedha kwa ajili ya masomo na mahitaji yake ya baadae.

Furahi usalama wa fedha zako na riba ya kuvutia! Wapigie 080011223 kwa maelezo zaidi ama tembelea tawi lolote la NMB lililo karibu yako. Follow @nmbtanzania na Facebook page ya NMB Tanzania #NMBJUNIORACCOUNT” aliweka Diamond kwenye kurasa wake kijamii wa Instagram.

Hii inafuatia muda mrefu kwa mtoto huyo kutowekwa kwa sura yake hadharani hali iliyozua utata kama ni wa Diamond ama la!!.. 


Ujio huu wa Tiffah kuanikwa wazi kwa watu wamuone ni baada ya kufikisha 40, tokea kuzaliwa kwake huku awali kampuni mbalimbali za ndani na nje ya Nchi zikiwania saini za wazazi wawili hao Diamond Platnumz na Zari ama Zari the Boss Lady.

Wapambe walonga!!
Katika kila jambo halikosi kasoro, tayari watu mbalimbali wakiwemo wapambe wa Diamond na mwanadada Zari the Boss Lady wameweza kusambaza picha hizo kwa kila aina ya njia huku habari ya mjini ikiwa ni mtoto Tiffah kuonyeshwa hadharani.
Tayari kurasa za mitandao ya kijamii za mwanamuziki Diamond, mama wa Tiffah, Zari na ukurasa wa Tiffah mwenyewe umeweza kupata Likes na Comments nyingi kutoka kwa fans wao ambao walikuwa na shahuku kubwa ya kumuona mtoto huyu huku wengine wakienda mbali kuwa mtoto kafanana na Mama na wengine wakieleza kuwa bado hawaamini kama ni mtoto wa Diamond ama la!
#Picha na MO Blog

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI