Friday, January 6, 2017

MEEK MILL AMCHANA NICKI MINAJ BAADA YA KUMWAGANA

Muda mfupi baada ya Nicki Minaj kutangaza kupitia Twitter kuwa ameachana na Meek Mill, rapper huyo amemchana demu wake huyo wa zamani kwenye Instagram.
Alhamis hii, Meek aliweka picha Instagram ya viatu vyeupe brand ya Giuseppe Zanotti zenye mistari ya dhahabu na kuandika, “If you walk out don’t wear these, they wack.”


Viatu alivyoviponda Meek ni vile ambalo Nicki Minaj alivivaa kwenye video ya wimbo wa mwaka 2013 alioshirikishwa na Ciara, I’m Out.
Wimbo huo una mashairi ya Minaj yanayosema, “You gon’ play me? / On Instagram, ni**as trying to shade me / But your bitch at home trying to play me.”

ANGALIA *PICHAZ* ZA JENNIFER NA PATRICK WA KANUMBA WALIVYOKUWA WAKUBWA

HUENDA ukakutana barabarani na Hanifa Daud ‘Jennifer’ pamoja na Othman Njaidi ‘Patrick’ ambayo ni zao la marehemu Steven Kanumba na usiwafahamu kwa jinsi walivyokuwa wakubwa.
Vijana hao wawili walifanya vizuri ndani ya filamu ya Uncle JJ pamoja na This Is It wakiwa na marehemu Steven Kanumba.
 Jennifer ambaye mwaka 2014 alionekana kwenye filamu ya Zena na Betina ya Salma Jabu aka Nisha, amehitimu kidato cha nne mwaka huu.

Kwa upande wa Patrick 2016 alihojiwa na mtandao mmoja wa habari nakudai hana mazuka wa kuigiza kwa sasa kama zamani.
Angalia picha zao hapa.








Q CHIEF AZUNGUMZIA KWANINI NGOMA ZAKE HAZIFANYI VIZURI PAMOJA NA MAPUNGUFU YA LABEL YA Q MHONDA

Q Chief akiwa na Mkurugugenzi wa Qs Mhonda Entertainment
Msanii mkongwe wa muziki Q Chief amedai kuwa kuna mambo ambayo anakosea kwenye muziki wake ndiyo maana ngoma zake kadhaa alizoziachia hivi karibuni zimeshindwa kufanya vizuri zaidi kama alivyotarajia.
Muimbaji huyo ambaye yupo chini ya label ya Qs Mhonda Entertainment, ameiambia Bongo5 kuwa hali hiyo imemfanya akae yeye pamoja na uongozi wake ili kulitafuta ufumbuzi suala hilo.
“Baada ya kufanya ngoma kadhaa nimeona kuna ulazima wa kukaa chini na uongozi wa management yangu na kuisukuma ijisukume zaidi kunisukuma kwa maana thamani ya uwekezaji wa audio na video unatakiwa kuwa sawa au zaidi na thamani na promotion pamoja na maisha halisi ya msanii ambayo anatakiwa kuishi,” alisema Q Chief.
Aliongeza, “Kwa hiyo mwaka 2017 ni mwaka ambao nataka kufanya mabadiliko makubwa sana, lakini kabla ya yote nataka marekebisho katika mkataba wangu na Q Mhonda kwa sababu una mapungufu mengi sana, na ningependa kuyarekebisha kwa lengo la kuweka mambo sawa,”
Pia muimbaji huyo amewashukuru mashabiki wa muziki wake kwa kuonyesha mapokezi mazuri katika wimbo wake mpya alioshirikiana na Patoranking wa Nigeria.

RIYAD MAHREZ ATUMA UJUMBE KWA MASHABIKI BAADA YA KUSHINDA TUZO

NI furaha kwa kila mtu pindi mchango wake unapoonekana na kupewa zawadi – ndicho kilichomtokea Riyad Mahrez usiku wa Alhamisi hii baada ya kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa kuwabwaga washiriki wengine akiwemo Pierre-Emerick Aubameyang na Sadio Mane.
Mahrez ambaye ni mchezaji wa Algeria amewashukuru mashabiki wote duniani kutokana na kuwa na msimu mzuri kwa mwaka jana na kufanikiwa kuisaidia timu yake ya Leicester City kushinda taji la ligi kuu ya Uingereza.
Kupiti kwenye mitandao yake ya kijamii, mchezaji huyo ameandika, “African ballon d’or … I thank everyone who supporte me around Africa and around the world .”
Hii ni tuzo ya tatu kubwa kushinda kwa mchezaji huyu baada ya ile ya ‘Mchezaji bora wa mwaka ya chama cha wachezaji soka ya kulipwa Uingereza (PFA) na ‘BBC African Player of the Year’.

ANGALIA *PICHAZ&VIDEO* ZA WACHEZA DANSI 50 WALIOFUNGA MTAA KWA KUTUMBUIZA JUU YA MAGARI KUSHEREHESHA MAZISHI YA MWANASIASA TAIWAN

WACHEZA DANSI wa kike kwenye kumbi za usiku wapatao 50, wakiwa wamevalia vivazi vyeusi wamewaacha na mshangao wapita njia wakati wakiusindikiza mwili wa mwanasiasa mmoja aliyefariki mwezi Decemba nchini Taiwan.

Kwenye msafara wanawake hao wakiwa juu ya magari ya aina ya “Jeep”, yenye rangi tofauti walikuwa wakicheza na kuimba na kusababisha foleni kubwa ya magari barabarani na watu wengi kubaki wakiwashangaa, kwa kuwa ni kinyume na tamaduni za huko.
Waendesha pikipiki nao waliufuatilia msafara wakiwashangaa wanawake hao. Familia ya mwanasiasa huyo imesema, marehemu Tung Hsiang aliagiza kufanyika namna hiyo, kwa kuwa alipendelea mambo kama hayo.
Angalia Picha zaidi hapa chini:



MAREKANI YAENDELEA NA MPANGO WA KUWAHAMISHA WAFUNGWA TOKA GUANTANAMO BAY

Mmoja kati ya wafungwa waliohamishwa kutoka Guantanamo Bay akisalimiana na ndugu zake
MAREKANI imewaachia baadhi ya wafungwa wa Yemen waliokuwa wakishikiliwa katika gereza la Guantanamo Bay nchini Cuba.
Makao makuu ya Pentagon yamethibitisha kuwahamisha wafungwa hao na kusema kuwa kwa sasa ni wafungwa 55 wamebakia katika gereza hilo. Mwandishi wa AFP amedai kuwa aliwaona wafungwa wanne wakishuka katika uwanja wa ndege wa Riyadh ambao umezoeleka kwa kutua viongozi wakubwa.
Baada ya kuwaona ndugu zao mmoja wa ndugu wa wafungwa hao, Mohammed Bawazir alisema, “I want to give back to my family the 15 years I lost.”
Hivi karibuni Marekani iliahidi kuendelea na mpango wake wa kuwahamisha wafungwa waliopo katika gereza la Guantanamo Bay kitendo ambacho kimekuwa kikipingwa vikali na Rais mteule wa nchi hiyo, Donald Trump.

BARUA ZA MKONO ALIZOANDIKA PRINCESS DIANA ZAUZWA KWA MAELFU YA POUND!

BARUA zilizoandikwa kwa mkono na marehemu Princess Diana zimeuzwa kwa maelfu ya pound kwenye mnada uliofanyika Alhamis hii nchini Uingereza.
Barua hizo sita zilitumwa kwa Cyril Dickman, aliyekuwa mwangalizi mkuu wa ikulu ya Buckingham miaka ya 1980 na 1990. Katika barua moja iliyotumwa siku tano baada ya kuzaliwa kwa Harry, September 1984, Diana alimshukuru Dickman kwa kadi aliyomtumia na kueleza jinsi Prince William alivyokuwa akimpenda mdogo wake.
“William adores his little brother and spends the entire time swamping Harry with an endless supply of hugs and kisses, hardly letting the parents near!” aliandika.
Barua hiyo iliuzwa kwa paundi 3,200. Diana alifariki kwa ajali ya gari mjini Paris mwaka 1997.

KUCHANGANYA POMBE NA VINYWAJI VYA KUONGEZA NGUVU (ENERGY DRINKS) NI HATARI KWA AFYA YAKO

MCHANGANYIKO wa pombe na vinywaji vya kuongeza nguvu vijulikanavyo kama Energy drinks vilitosha kumfanya akose usingizi na kuwa mwenye nguvu kwa muda wote kipindi alipokuwa akikesha katika kumbi tofauti tofauti za starehe katika katika jiji la Dar es Salaam wakati akisoma katika chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Lakini leo hii akizungumzia mambo yanayohusu afya yake na yako, kuchanganya pombe na Energy drinks ni jambo ambalo asingekushauri kabisa ulifanye. Kwani hali ya afya yake ipo ukingoni na asingependa kabisa kuona mtu mwingine akiingia katika majanga aliyoyapata yeye.
Je ni kweli vinywaji hivi vijulikanavyo kwa jina la energy drinks huongeza nguvu kama inavyosemekana? Wataalam wa afya wanatoa tahadhari kuhusiana na madhara yatokanayo na hivi vinywaji maarufu. Utumiaji wa vinywaji hivi kwa muda mrefu husababisha matatizo ya moyo ambayo ni hatari sana kwa afya yako.
Utafiti uliofanyika katika nchi nyingi duniani unaonyesha vinywaji hivi vikitumiwa kwa muda mrefu huleta madhara makubwa kwa watumiaji kama vile kuongezeka kwa mapigo ya moyo (Increased heart rate) ambayo hupelekea kuongezeka kwa msukumo wa damu (blood pressure) ambapo mwisho wa siku hupelekea watumiaji kupata shinikizo la moyo (Hypertension) na shambulio la moyo(heart attack).
Kitaalam vinywaji hivi vijulikanavyo kama energy drinks vimechanganywa na caffeine ambayo husababisha mnywaji wa vinywaji hivi kukosa usingizi huongeza uelewa na hupunguza uzito.
Lakini ikitumiwa kwa wingi na kwa muda mrefu, caffeine husababisha addictions na matatizo ya moyo. Kwahiyo ni vema tukaepuka kuchanganya pombe na vinywaji vya aina hii ili kuepukana na madhara yatokanayo na utumiaji wa mchanganyiko huu.
IMEANDIKWA NA:
FORD A. CHISANZA
Intern pharmacist
Tanzania Food And Drug Authority (TFDA)
Mobile:+255 652466430/+255 684363584
Email: fordchisanza@gmail.com

DAYNA NYANGE ACHAGULIWA KUWANIA TUZO ZA BAE AWARDS ZA NIGERIA

MSANII wa Bongo Fleva, Dayna Nyange amechaguliwa kuwania tuzo za BAE Awards 2017 za nchini Nigeria akiwa ni msanii pekee kutoka Tanzania.
Hitmaker huyo wa Komela amechaguliwa katika vipengele viwili ikiwemo kimoja cha BEST AFRICAN ACT akichuana na Eddy Kenzo (Uganda), King Kaka (Kenya), Stoneboy (Ghana), Jah Vinci (Jamaica).
Kipengele kingine anachowania ni BEST VOCAL PERFORMANCE FEMALE kupitia wimbo wake ‘Angejua’ ambapo anawania tuzo hiyo na Aramide, Ngowari na Rocknana (wote kutoka Nigeria).

UJUMBE WA SAMATTA ALIOMUANDIKIA NDINDI BAADA YA KUTUA LEICESTER CITY

Mbwana Samatta akiwa na Ndidi katika timu ya KRC Genk
Nahodha wa timu ya taifa Tanzania (Taifa Stars), Mbwana Samatta ambaye anacheza katika klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji amemuandikia ujumbe wa kumtakia kila la kheri mchezaji mwenzake Wilfred Ndindi ambaye amesajiliwa na Leicester City ya Uingereza.
Kiugo huyo wa zamani wa Genk alitambulishwa rasmi na mabingwa hao watetezi wa taji la ligi Kuu Uingereza akiwa kama mbadala sahihi wa Ng’olo Kante aliyejiunga na Chelsea mwanzoni mwa msimu huu.
Imedaiwa kuwa mchezaji huyo amesajiliwe kwa dau la Paundi milioni 15.
Huu ndio ujumbe wa Samatta alimuandikia mchezaji huyo

WAJERUMANI WASHAURIWA KUTEMBEA KAMA NDEGE PENGUIN ILI KUJIKINGA NA AJALI

MADAKTARI nchini Ujerumani wamewashauri raia kutembea kama ndege aina ya Penguin kwa lengo la kuepuka kuteleza na kuanguka katika kipindi hiki cha baridi jambo linalotokana na kuganda kwa barafu baraabarani.
Madaktari nchini Ujerumani wamewashauri raia watembee kama ndege aina ya penguin katika kipindi hiki cha baridi kali lenye kuandamana na kuanguka kwa theluji ambazo baadae zinaganda na kuwa barafu katika maeneo mengi ya barabara.
Kitengo cha utabiri wa hali ya hewa kimesema hali hiyo itaendelea kwa siku kadhaa na kwamba aina hiyo ya kutembea inayomsadia kiumbe huyo anaeishi katika maeneo ya baridi kali, inaweza kuwanusuru watu na hatari ya kuvunja viungo vyao.
Ushauri huo uliosambazwa kupitia tovuti ya chama cha watoa tiba ya mifupa nchini Ujerumani na ushauri na nasaha unasema kutembea kwa kunyata kunakufanywa na aina ndege huyo, kunaweza kusaidia kukabiliana na kuteleza katika barabara zenye barafu. Lakini kama binadamu atatembea kwa namna yake ya kawaida ni rahisi kuteleza na kuanguka.
Manispaa ya Berlin ilikosolewa vikali mwaka 2014 kwa kushindwa kumwagia chumvi maalumu zenye kusaidia kuyeyusha barafu katika njia nyingi, na hivyo kusababisha idadi kubwa ya watu kuteleza na kuumia.
Timu ya uokozi katika jiji hilo ilipokea simu za dharura 750 na vyumba vyake vya matibabu vilizongwa na idadi kubwa ya watu wenye matatizo ya mifupa. Na kwamba utabiri wa hali ya hewa wa sasa unaonesha kiwango cha joto kitashuka hadi kufikia hadi nyuzi joto -10.

JCB - 'KUFANYA KAZI NA MSANII WA BONGO FLEVA SI KITU KIBAYA'

RAPPER JCB amewapa somo wasanii wa Hip Hop na wadau wengine wasiopenda kuona msanii wa muziki huo akiachia wimbo wa pamoja na msanii wa Bongo Fleva.
JCB amekiambia kipindi cha Ladha 3600 cha EFM Alhamisi hii kuwa msanii wa Hip Hop akifanya kazi na msanii mwingine anayefanya muziki tofauti na huo haimaanishi ndio ameusaliti muziki huo.
“Kufanya Kazi na msanii wa Bongo Fleva haimaanishi umeisaliti Hip Hop,” amesema JCB.
Hivi karibuni msanii huyo anatarajia kuachia wimbo wake mpya alioupa jina ‘Tumeula Gang’.

EL HADARY KUWEKA REKODI MICHUANO YA AFCON 2017

GOLIKIPA mkongwe wa Misri Essam El Hadary huenda akaibuka mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kucheza katika fainali za Kombe la Mataifa bingwa Afrika baada ya kutajwa kwenye kikosi kitakachowakilisha taifa hilo Gabon.
El Hadary anatimiza miaka 43 mwezi huu na yumo kwenye kikosi cha wachezaji 23 wa Misri watakaosakata gozi Gabon.
Rekodi ya sasa inashikiliwa na Mmisri mwingine Hossam Hassan aliyecheza mwaka 2006 akiwa na miaka 39.
Kocha wa timu ya taifa Hector Cuper aliwaondoa wachezaji wanne kutoka kwenye kikosi shikilizi na kusalia na kikosi chake cha mwisho.
Waliotemwa na beki Hamada Tolba na kiungo wa kati Ahmed Gomaa wa Al Masry, kiungo wa kati wa Zamalek Mohamed Ibrahim na kipa wa Ismaili Mohamed Awad.
Ni wachezaji wanne pekee wa kikosi cha Misri kilichocheza fainali za mwisho walizoshiriki mwaka 2010 ambapo walifanikiwa kutwaa kombe hilo mara ya tatu mtawalia.
Wachezaji hao ni El Hadary, Ahmed Elmohamady, Mohamed Abdelshafi na Ahmed Fathi.
Misri, ambao walikosa fainali tatu zilizopita, wamo Kundi D ambapo watafungua kampeni yao dhidi ya Mali mnamo tarehe 17 Januari dhidi ya Mali.
Michuano hiyo itachezewa Gabon 14 Januari hadi 5 Februari.
Kikosi cha Misri
Walinda lango: Sherif Ekramy (Al Ahly), Essam El Hadary (WadiDegla), Ahmed El Shennawi (Zamalek)
Mabeki: Mohamed Abdelshafi (Al Ahly Jeddah), Ahmed Dwidar(Zamalek), Ahmed Elmohamady (Hull City), Ahmed Fathi (Ahly),Omar Gaber (FC Basle), Ali Gabr (Zamalek), Karim Hafez (RacingLens), Ahmed Hegazy, Saad Samir (both Al Ahly)
Viungo wa kati: Mohamed Elneny (Arsenal), Abdallah El Said (AlAhly), Mahmoud Trezeguet Hassan (Royal Mouscron-Peruwelz), TarekHamed, Ibrahim Salah (both Zamalek), Amr Warda (Panetolikos)
Washambuliaji: Mahmoud Abdelmoneim Kahraba (Al Ahly Jeddah),Ahmed Hassan Kouka (Sporting Braga), Marwan Mohsen (Al Ahly),Mohamed Salah (Roma), Ramadan Sobhi (Stoke City).
#BBC

WAWILI WAHUKUMIWA KWENDA JELA CHINA KWA KUFUNGUA BENKI BANDIA NA KUWATAPELI WATU 400

MAHAKAMA mjini Nanjing, China, imewafunga jela wanaume wawili waliowatapeli wateja kupitia benki bandia, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti.
Wanaume hao waliotambuliwa kwa majina Zeng na He, walipatikana na makosa ya kujipatia yuan 435m (£51m; $63m) kutoka kwa wateja 400.
Hukumu dhidi yao ilithibitishwa baada ya kesi dhidi yao kurudiwa, gazeti la People’s Daily limeripoti.
Walianzisha chama cha ushirika ambacho afisi yake ndani zilifanana na za benki moja inayomilikiwa na serikali.
Walikuwa na madawati na makarani wenye sare zilizofanana na makarani rasmi wa benki ya serikali.
Hata stakabadhi za kuweka amana pesa kwenye benki zilikuwa sawa na za benki ya serikali.

Lakini ingawa taasisi hiyo ilikuwa na kibali cha kuhudumu kama chama cha ushirika, haikuwa na kibali cha kuhudumu kama benki.
Wahudumu waliwavutia wateja kwa kuwaahidi viwango vya juu vya riba kwa pesa walizoweka amana.
Shughuli haramu za taasisi hiyo ziligunduliwa mfanyabiashara aliyekuwa ameahidiwa riba ya juu alipodai riba aliyoahidiwa lakini akakosa kulipwa na akapiga ripoti kwa maafisa wa polisi mwaka 2014.
Ni baada ya hapo ambapo uchunguzi wa kina ulianzishwa.