Monday, October 31, 2016

MSANII MABESTE NA MENEJA WAKE LISA FICKENSCHER WAFUNGA NDOA *PICHAZ*

 Msanii wa muziki wa hip hop Mabeste weekend hii amefunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu aitwae, Lisa Fickenscher.
Wawili hao tayari wana mtoto mmoja aitwae, Kendrick Mabeste.
Kupitia instagrm, Mabeste ameandika:
Morning .. Hatimae nimeopoa Jana 😄😄Thank you sana My Big brother Jesus And Thank you
Rapa huyo amekuwa ni miongoni mwa wasanii wa bongofleva waliofunga ndoa mwezi huu baada ya Tunda Man pamoja Nyandu Tozzy kufunga ndoa siku chache zilizopita. Angalia picha.

DARASSA ADAI KUJA NA COLLABO NA CHRISTIAN BELLA

Rapper Darassa amefunguka kuwa muda si mrefu atakuja na collabo yake na Christian Bella.
Akiongea na kipindi cha Clouds Top 20 cha Clouds FM, Darassa amesema kuwa amefurahi kusikia kuwa Bella anamkubali sana kwa hiyo mashabiki watarajie kazi yao ya pamoja.
“Jana [Jumamosi] tulikuwa tumekaa sehemu nikasikia mtu anasema kuwa Christian Bella ananikubali sana, hata mimi ni shabiki wake mkubwa. Tumepanga kufanya collabo, mashabiki wasubirie kitu kikubwa,” amesema Darassa.

Kwa sasa Darassa ni mmoja kati ya rapper wa kizazi kipya ambao kazi zao zinafanya vizuri kwenye Redio na TV mbalimbali.

IYANYA ASAINISHWA NA MAVIN RECORDS YA DON JAZZY

Himaya ya Mavin Records imemsanisha msanii heavy weight, Iyanya. Mkali huyo anaungana na orodha iliyoshiba ya Mavin inayojumisha wakali kama Tiwa Savage, Dr SID, D’Prince, Di’Ja, Korede Bellona Reekado Banks.
Katika kumtambulisha Iyanya kwenye label yake, Don Jazzy ameandika kwenye Instagram: The SUPREME MAVIN DYNASTY is pleased to welcome @Iyanya to the ever growing Mavin Family. Pls join us to welcome him and let the world know that we #Up2Sumting. #MavinActivated.
Naye Dr Sid ameandika: I’m happy to welcome @iyanya to @mavinrecords as the newest member of the #Mavin family #SMD #UP2SOMETHING #MAVINACTIVATED Happy birthday bro
Dili hili limekuja miezi mitatu baada ya Iyanya kuachana na meneja na mshirika wake wa miaka 6 Ubi Franklin waliyekuwa na label yao, MMMG. Alikuwa na mpango wa kuanzisha label yake.
Tayari Iyanya ameachia wimbo Up To Something akiwashirikisha Don Jazzy & Dr Sid.

Ji

WEMA SEPETU AMUANDIKIA UJUMBE MISS TANZANIA MPYA

Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu amedai mshindi wa shindano la Miss Tanzania 2016, Diana Edward alistahili kuchukua taji hilo.
Kupitia Instagram, Wema ameandika:
When You Nailed that question Properly, I knew that The Crown was Yours…. Congratulations mdogo wangu… You deserve it… And I have a very good feeling about Your performance in the Miss World Beauty Pageant…. You will do Tanzania Proud… @dianaflave @dianaflave @dianaflave @dianaflave … #GoodMorningWorld
Faraja Nyalandu aliyewahi kushika taji hilo naye amekuwa miongoni mwa watu waliompongeza mshindi huyo.

UTALII WA NDANI: MAKONDA AZINDUA NEMBO ‘I LOVE DAR’

Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda amezindua nembo ya I love Dar (naipenda Dar) inayobeba dhana nzima ya utalii wa ndani hususan mkoa wa Dar es Salaam.
Tukio hilo lilotokea juzi usiku majira ya saa saba huku likishuhudiwa na mamia ya watu waliojitokeza kwenye uzinduzi huo uliofanyikia katika baa ya Element iliyopo Oyster bay.
Akizungumza baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi wa nembo hiyo Makonda alisema kuwa ni hatua nzuri kwa wadau binafsi kujitokeza na kuendeleza mazuri kwa Mkoa wa Dar es Salaam.
Alisema kuwa kwa kupitia nembo hiyo ya I love Dar inahamasisha kuendeleza uzuri wa Mkoa wa Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na kutangaza kila aina ya kivutio chake.
Alisema, vipo vitu vya asili ambavyo vinatumiwa kama utalii hasa kuanzia majengo ya kizamani hasa maeneo na mjini, makumbusho za taifa zenye kuhifadhi historia ya Mkoa pamoja na mengineo.
Alisema kuwa nembo hiyo inaenda mbali hadi kuhamasisha masuala ya kimaendeleo ya Dar es Salaam likiwamo suala zima la usafi pia.
“Najua I Love Dar ni nembo ambayo inamaana kubwa sana kwa wananchi kwa ujumla kuipenda Dar ni pamoja na kufanya mazuri kwa ajili ya Mkoa huu hapo ikiwa ni suala zima la kutangaza vivutio, kuzingatia usafi na mengine yote mazuri” alisema Makonda.
Kwa upande wake Meneja wa Baa ya Element, Mackenzie alisema kuwa katika kuhakikisha kuwa inaunga mkono sera ya kuendeleza utalii wa ndani imeamua kuanzia kwa kubuni nembo hiyo.

Alisma hata katika majiji makubwa duniani kama vile New York ina nembo ya I love New York na kwa hapa nchini kuandika I love Dar ni mwanzo wa kuliendeleza jiji la Dar kwa kuanzia kwenye Utalii.

BEYONCE, KELLY ROWLAND NA MICHELLE KUIRUDISHA DESTINY’S CHILD?

Mashabiki wa kundi la Destiny’s Child wameanza kupata mshtuko baada ya kuona dalili zinazoonyesha kuonekana kurudi tena kwa kundi hilo. Hii ni ndoto ya muda mrefu kwa mashabiki wa kundi hilo.
Mshtuko mkubwa ulianza kuibuka wiki iliyopita baada ya kuonekana kufunguliwa kwa akaunti mpya ya mtandao wa Instagram inayotumia jina la kundi hilo ambayo mpaka sasa imefanikiwa kupata follower’s 32.2k na kuwa verified kwa muda mfupi zaidi.

PAKUA NA UIANGALIE BRAND NEW VIDEO YA GODZILLA FT MAUA SAMA - YOUR BODY

Wakuitwa Godzilla humu ndani katika Your Body amefanya uhalifu wa kutosha na Maua Sama ndio mshirika wake.
Aisseeeee nimeona sio mbaya nikusogezee kichupa chake kipyaaa.
Kumbuka kama nawe pia ni msanii au una rafiki, ndugu, jamaa ambaye ungependa kuiona kazi yake kupitia mtandao huu basi wasiliana nasi kupitia
 # +255 715 002 890
Email: ulimwengu.habari@gmail.com

ANGALIA BRAND NEW VIDEO YA FEMI ONE - PILAU NJERI


Unaweza muita Femi One, nimekusogezea hapa kichupa chake kipyaaaa..
Kama pia wewe ni msanii na ungependa kazi yako unapenda ionekane kupitia mtandao wetu, wasiliana nasi kwa # +255 715 002 890
Email: ulimwengu.habari@gmail.com
utapata furusa ya kazi yako kuonekana!

MANISPAA YA ILALA JIJINI DAR KUWAONDOA WAFANYABIASHARA WOTE WALIO KANDO KANDO YA BARABARA ZA MWENDO KASI

HALMASHAURI ya manispaa ya Ilala jijini DSM kesho inaanza rasmi Operesheni ya kuwaondoa wafanyabiashara wote wanaoendesha biashara kando ya barabara za mwendo kasi kuanzia eneo la Gerezani Kariakoo hadi Fery Kivukoni kwa kuwa kufanya hivyo ni kwenda kinyume cha sheria mbali ya kusababisha usumbufu na ajali kwa watembea kwa miguu.

Mkuu wa wilaya ya Ilala Sofia Mjema akizungumza na waandishi wa habari amesema zoezi hilo litaanza mapema asubuhi na kuwataka wafanyabiashara hao kwenda katika maeneo waliyopangiwa ikiwemo soko Mburahati, Kigogo Sambusa na maeneo rasmi yaliyoainishwa.

Katika eneo la kariakoo chanel ten imeshuhudia adha kubwa kwa wananchi wanaotembea kwa miguu ambapo wanalazimika kupita katikati ya barabara ya magari ya mwendo wa haraka huku magari hayo yakipita kwa kasi na kuhatarisha maisha yao kutokana na wafanyabiashara hao kupanga biashara zao katika njia za watu wanaotembea kwa miguu.

SERENGETI NA BUNDA WANUFAIKA NA UWEKEZAJI WA SINGITA GRUMETI

Mkurugenzi wa Singita Grumeti Stephen Cunliffe (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk. Charles Mlingwa msaada wa madawati 500 yenye Thamani ya Tshs Milioni 112 kwa ajili ya Wilaya za Serengeti na Bunda katika hafla iliyofanyika Shule ya Msingi Makundusi Wilayani Serengeti.
Mkurugenzi wa Singita Grumeti Stephen Cunliffe (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk. Charles Mlingwa msaada wa madawati 500 yenye Thamani ya Tshs Milioni 112 kwa ajili ya Wilaya za Serengeti na Bunda katika hafla iliyofanyika Shule ya Msingi Makundusi Wilayani Serengeti.
Mkurugenzi wa Singita Grumeti Stephen Cunliffe (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk. Charles Mlingwa msaada wa madawati 500 yenye Thamani ya Tshs Milioni 112 kwa ajili ya Wilaya za Serengeti na Bunda katika hafla iliyofanyika Shule ya Msingi Makundusi Wilayani Serengeti.
Madawati yaliyotolewa na Mfuko wa Singita Grumeti kwa ajili ya Wilaya ya Bunda.

Mfuko wa Singita Grumeti umeendelea kuwa mstari wa mbele katika kuboresha hali ya elimu katika Wilaya za Serengeti na Bunda.

Hii imedhihirika kwenye halfa ya kukabidhi madawati 500 kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk. Charles Mlingwa ili kupunguza uhaba wa madawati katika Wilaya hizo. Aidha Grumeti wamekabidhi nyumba ya kuishi mwalimu iliyojengwa katika Shule ya Msingi Makundusi.

“Tuko hapa kukabidhi madawati haya 500 yenye thamani ya Tshs Milioni 112 kwa Wilaya za Serengeti na Bunda pamoja na nyumba hii yenye thamani ya Tshs Milioni 86” alisema Richard Ndaskoi ambae ni Mkuu wa Huduma za Jamii toka Mfuko wa Singinta Grumeti.

Akipokea misaada hiyo, Dk. Mlingwa alisema “Nawashukuru Singita Grumeti kwa Msaada huu wa madawati pamoja na nyumba hakika mchango wenu katika Mkoa wa Mara unaoneka” Dk Mlingwa amewataka wawekezaji wengine katika Mkoa wa Mara kuchangia madawati katika Wilaya za Serengeti na Bunda kwani bado zina uhaba wa madawati. 

Aidha Dk. Mlingwa ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti kwa kuwa na mahusiano mazuri na wawekezaji waliopo katika Wilaya hiyo “Tukiwawekea mazingira mazuri ya kufanya shughuli zao hata wananchi pia watanufaika na uwepo wa wawekezaji hawa” alisema Dk. Mlingwa. 

Naye Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili wote kwa nyakati tofauti wameushukuru Mfuko wa Singita Grumeti kwa msaada huo wa madawati na kuuomba mfuko huo kuendelea kuchangia katika shughuli za maendeleo katika Wilaya za Serengeti na Bunda. “Wilaya hii ina wawekezaji wengi lakini wamekuwa nyuma katika kuchangia shughuli za maendeleo, nawapongeza kwa kuwa mstari wa mbele kusaidia jamii inayowazunguka pamoja na kuchangia katika maendeleo ya Wilaya ya Serengeti” alisema Nurdin Babu.

Aidha Bi. Bupilipili ameuomba Mfuko huo kuanzisha kampeni maalumu ya kuongeza kiwango cha ufaulu kwa watoto wa kike kwa shule za sekondari Wilayani Bunda.

Singita Grumeti wamekuwa wawekezaji wenye tija kwa wananchi wa Wilaya za Serengeti na Bunda licha ya kuwa mstari wa mbele kuchangia katika shughuli za maendeleo, kampuni hiyo pia imekuwa ikitoa ajira kwa wakazi toka wilaya hizo mbili pamoja na kutoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi toka wilaya hizo.
ENGLIBERT THOMAS KAYOMBO
AFISA HABARI NA MAHUSIANO
HALMASHAURI YA WILAYA YA SERENGETI

KIFO CHA MUUZA SAMAKI CHAZUA MAANDAMANO MOROCCO

Picha: Reuters.
Maandamano baada ya muuza samaki kukanyagwa na lori hadi kufa nchini Morocco
Maelfu wa raia wa Morocco walifanya maandamano wikendi hii katika miji kadhaa baada ya muuza samaki mmoja kukanyagwa hadi kufa na lori la kubeba takataka alipokuwa akijaribu kuchukua samaki wake ambao alikuwa amepokonywa na maafisa wa polisi.
Kifo cha Maouhcine Fikri katika mji wa kaskazini wa Al-Houciema siku ya Ijumaa kilizua hasira kali miongoni mwa raia katika mitandao ya kijamii.
Kifo chake kinafananishwa na kile cha muuza matunda wa Tunisia mwaka 2010 ambacho kilisababisha maandamano makubwa.
Mfalme wa Morocco King Mohammed VI amewaagiza maafisa wake kutembelea familia ya Fikri.
Wizara ya maswala ya ndani pamoja na ile ya Haki zimeahidi kuanzisha uchunguzi.
#BBC Swahili

Saturday, October 29, 2016

NEW COUPLE IN TOWN: MPENZI MPYA WA LINAH MMMH!

Ule usemi wa Kiswahili unaosema ‘penzi ni kikohozi kulificha hauwezi’ unazidi kujidhihirisha kwa malkia wa muziki Linah Sanga baada ya kumweka wazi mpenzi wake mpya ikiwa miezi 6 toka adai hatoweka tena mahusiano yake wazi.
Linah akiwa na mpenzi wake
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Raha Jipe Mwenyewe’ mapema mwaka huu alidai kuweka wazi mahusiano yake ya mapenzi kunamwaribia muziki wake kutokana na mashabiki wake kupenda kufuatilia mambo yake ya ndani kuliko muziki wake.
Ijumaa hii muimbaji huyo ambaye pia aliwahi kutoka kimapenzi na Barakah The Prince ameamua kumweka wazi mpenzi wake mpya.
“Penzi sio kama nyanya itokayo sokoni, nipe penzi mwanana niliote ndotoni. I love u cheusi wangu @director_ghost #maramojamojasiyombaya #rahajipemwenyewe,” Linah aliandika istagram kupitia hiyo picha hapo juu.

Muimbaji huyo ni moja kati ya waimbaji wa kike ambao wanafanya vizuri katika tasnia ya muziki.

JAH PRAYZAH AMSHUKURU DIAMOND KWA KUMWEKA KWENYE RAMANI YA AFRIKA

Ukishikwa mkono na waliokutangulia na wewe shika wengine walio nyuma yako.
Davido kupitia Number One Remix, alimtambulisha Diamond kwenye ramani ya Afrika. Baada ya miaka michache, Diamond pia amefanikiwa kuwatambulisha zaidi wasanii wengine kwenye jicho pana la muziki wa bara hilo.
Miongoni mwao ni Akothee wa Kenya na Jah Prayzah wa Zimbabwe.
Jina la Prayzah limekuwa kubwa nje ya Zimbabwe mwaka huu baada ya kumshirikisha Diamond kwenye wimbo wake Watora Mari. Kama hiyo haitoshi, muimbaji huyo hivi karibuni alishinda tuzo ya MTV MAMA (Listener’s Choice) – na anadhani haijaja kwa bahati mbaya bali Diamond amechangia.
Amemweleza Diamond kama ni mtu wa pekee.

“Big shout out to @diamondplatnumz,” ameandika kwenye Twitter. “It’s no coincidence that in the same year Watora Mari made waves, I got the MAMA award. You are amazing.

MIMI NI RAPPER PEKEE BONGO NINAYESHINDANA NA WASANII WA KUIMBA – MR BLUE

Mr Blue amedai kuwa yeye ndio rapper pekee anayeshindana na wasanii wanaoimba.
Rapper huyo amesema hayo kwenye kipindi cha Friday Night Live cha EATV wakati akifafanua sababu ya kutumia aka nyingine siku za hivi karibuni ‘Most Expensive MC’.
“Unajua mimi ndio rapper pekee ninayeshindana na wasanii wa kuimba. Ukiachilia mbali kwa mali nazomiliki lakini hata mashairi yangu, ninaweza nikakaa mwaka mzima nikatoa nyimbo mmoja au mbili na zikafanya vizuri ndani ya mwaka huo wote,” amesema Blue.

Kwa sasa Blue ni mmoja kati ya wasanii wa Bongo wenye aka nyingi zaidi ikiwa ni zaidi ya tano.

ANGALIA VIDEO MPYA YA ABBY SKILLZ FT ALIKIBA & MR BLUE - AVERINA

Baada ya kimya kirefu, msanii mkongwe wa Bongo Fleva Abby Skillz ameachia video ya wimbo wake mpya wa ‘Averina’ aliomshirikisha Alikiba na Mr Blue. Video hiyo imeongozwa na director Pablo. Tazama video hiyo hapa chini.

HAPPY BIRTHDAY RAIS WA TANZANIA MAGUFULI

IKIWA leo ni siku ya kuzaliwa ya Rais Dkt John Magufuli  watu wa fani na rika mbalimbali wameendelea kumpongeza kupitia mitandao ya kijamii.
“Ninamshukuru Mungu kufikia siku yangu ya kuzaliwa,ninawashukuru watanzania nyote kwa kuniombea,” ameandika kwenye Twitter. “Nitafanya kazi kwa moyo nanguvu zangu zote,” ameongeza.
“Ninaahidi kuendelea kufanya kazi kwa moyo na nguvu zangu zote kwa ajili ya maendeleo ya Taifa. Mungu Ibariki Tanzania.”
ULIMWENGU WA HABARI tunasemaaaaaa
"Happy Birthday mheshimiwa Rais Magufuli"

DUMA WA SIRI YA MTUNGI KUACHIA ‘CHUN’TAMA’ AKIWA NA MASTAA KIBAO

Msanii wa filamu Daudi Michael Tairo, anayefahamika zaidi kwa jina la Duma ndani ya tamthilia ya Siri ya Mtungi, amejipanga kuachia filamu yake mpya iitwayo ‘Chun’tama’.
Mwigizaji huyo ameiambia Bongo5 kuwa filamu hiyo itakuwa inazungumzia maisha halisi wa watanzania pamoja na masuala ya uchawi.
“Baada ya kufanya vizuri katika filamu yangu ya ‘Mchongo Sio’ nikaona nisikae kimya sana. Kwahiyo nimeamua kuachia filamu mpya inaitwa Chun’tama. kwenye filamu hiyo kuna mastaa kibao, Grace Mapunda, Chuchu Hans, Hashim Kambi, Barafu Suleiman na wengineo kibao. Na filamu inamatukio mengi pamoja na mambo yakichawi ndani yake,”

Pia mwigizaji huyo amesema hataki kuwaangusha mashabiki wake wa filamu ndiyo maana hataki kukaa muda mrefu bila kuachia filamu mpya.

ANGALIA VIDEO MPYA YA IBRAHNATION – NILIPIZE

MSANII Ibrahnation baada ya kufanya na audio ya wimbo “Nilipize”, ameachia video mpya ya wimbo huo angalia hapa, video imeongozwa na Geneouz Jeff.

BEN POL: SI LAZIMA KUMSHIRIKISHA MTU ILI WIMBO UWE MKUBWA

Mkali wa muziki wa RnB, Ben Pol amefunguka sababu inayoweza kuufanya wimbo ukawa mkubwa.
Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio kuwa wimbo ukiwa mzuri ni rahisi kuhit hata usipomshirikisha msanii mkubwa.
“Kinachoboost wimbo si msanii bali ni wimbo wenyewe. Ukiangalia ‘Moyo Mashine’ nimeimba mwenyewe umekuwa mkubwa, ‘Sofia’ niliimba mwenyewe lakini wimbo ulikuwa mkubwa sana,” amesema Ben.
Ben Pol ameongeza kuwa kuwashirikisha wasanii wenye majina makubwa hakufanyi wimbo ukapendwa zaidi ila ufundi uliotumika kwenye wimbo wenyewe ndio utaufanya wimbo huo kupendwa. Kwa sasa wimbo wa ‘Moyo Mashine’ umeendelea kufanya vizuri kwenye redio na TV japo una zaidi ya miezi mitano tangu utoke.

UTAFITI: KUKUMBATIWA NA UMPENDAYE WAKATI WA MAUMIVU KUNA NGUVU ZAIDI YA PARACETAMOL

Kumbatio kutoka kwa mtu umpendaye, linaweza kuwa na nguvu zaidi ya Paracetamol pale unapokuwa na maumivu, kwa mujibu wa utafiti.
Wanasayansi wamebaini kuwa hisia za ukaribu tunazozipata kupitia mtu anayetushika, kunaweza kusaidia kupunguza maumivu. Lakini kushikwa na mtu usiyemjua, kunaweza kusiwe na matokeo yale yake, kwasababu hatuna hisia nao.
Utafiti huo unaonesha nguvu ya ubongo kuzuia hisia za maumivu. Utafiti huo ulifanywa na wataalam katika chuo kikuu cha Haifa, Israel na ulihusisha wanawake kadhaa ambao waliwatengenezea maumivu kwa kuwaunguza na chuma chenye moto kiasi.
Katika jaribio la kwanza, mtu wasiyemjua aliwashika mkono akijaribu kuwaliwaza kwa maumivu hayo. Kwenye la pili waliwaita waume na wapenzi wao kukaa karibu nao na kugusanisha ngozi.
Katika jaribio la mwisho, wapenzi wao waliruhusiwa kuwashika mkono wakati chuma hicho cha moto kikigusishwa kwenye ngozi zao. Wanasayansi walibaini kuwa mguso wa mtu wasiyemjua pamoja na kuwa na mpendwa wao karibu hakukuwa na tofauti katika jinsi walivyosikia maumivu.
Lakini pale mtu wanayempenda alipowagusa kwenye ngozi, maumivu yalipungua.
Walibaini pia kuwa kadri mpenzi wa mwanamke alivyoonesha huruma na support kwake wakati wa zoezi hilo, alipata afueni zaidi.

NYIMBO 5 ZA BONGO FLAVA ZENYE UJUMBE AMBAO SI RAHISI MSANII WA LEO KUUFIKIRIA

Muziki ni sanaa, na sanaa ni ubunifu na upekee. Tasnia ya muziki wa Bongo flava ina miaka zaidi ya 20 sasa na kiukweli tasnia hii imepiga hatua kubwa sana kimaendeleo. Ndani ya kipindi chote hicho cha miaka zaidi ya 20 tumeshuhudia uwepo wa wasanii wengi wenye vipaji maridhawa na nyimbo zenye tija na ubunifu na upekee wa hali ya juu sana ambazo pengine kama wao wasingeimba basi zisingekuwepo kabisa.
Kwa mtazamo wangu, hizi ni nyimbo 5 za Bongo Flava zenye ubunifu usio rahisi kufanyika sasa
ALIKUFA KWA NGOMA – MWANA FA
Ni nyimbo ya pekee, ubunifu na utofauti ni wa hali juu. Meseji ya nyimbo hii ni tofauti sana na nyimbo nyingine zote zenye ujumbe kuhusiana na gonjwa hatari la UKIMWI. Wasanii wengi walioimba kuhusu UKIMWI walionesha kua starehe na uasherati ndio kama chanzo pekee cha gonjwa hili lakini Hamisi Mwinjuma ‘Mwana FA’ akasema hapana hata wacha Mungu na wafuasi wa maadili wanaweza kuathirika na gonjwa hili.
NDIYO MZEE NA SIYO MZEE – PROF JAY
Mbunge wa sasa wa jimbo la Mikumi, Mheshimiwa Joseph Haule alikuwa hashikiki enzi zake. Idea za siasa zilikuwa kichwani mwake muda mrefu. Nyimbo hizi mbili ni kama Part One na Part Two. Ndiyo mzee anaomba kura kwa wananchi ambao walimuamini na kumpa uongozi na Siyo Mzee ni kipindi kingine cha uchaguzi ambacho wananchi wanaonesha kumtosa baada ya kutotimiza ahadi zake za awali. Kwa ubunifu huu sioni kama kuna msanii mwingine angeweza kuimba hizi nyimbo kama Profesa Jay asingeimba.
NJE YA BOX - NICK WA PILI
‘Nje ya kumi na nane, nje nje nje ya box, nje ya kumi na nane’ hii ni chorus ya wimbo huu maridadi kabisa wa Hip hop ulioimbwa na kijana wa Hip Hop wa kizazi cha sasa Nick wa Pili akiwashirikisha members wenzake wa Kundi la Weus, kaka yake Joh Makini na G-Nako. 44
Kama ilivyo kwa jina la wimbo hata idea yake kweli ni nje ya box. Kikawaida kwa jamii yetu ya Tanzania na Afrika kwa ujumla wanaume wengi hupenda kuwa wanawake wanaowapenda katika shida na raha na si raha peke yake. Nick aliniacha hoi katika wimbo pale aliomba Mungu amjalie demu mpenda pesa ni kitu cha tofauti sana na ameenda na kinyume na mawazo ya wengi akiwepo Mr Blue aliyeimba ‘nipende kama nilivyo’. Kwa utofauti na ubunifu nisingetegemea kusikia idea hii kutoka kwa mwanamuziki mwingine kama Nick asingeimba.
JUA NA MVUA – JAY MOE
Anajiita Jay Moe Famous. Mimi hupenda kumuita mfalme wa Sinza. Wakati sisi wengine tukichukulia jua na mvua kama mabadiiko ya hali ya hewa tu ambayo ni matokeo ya dunia kulizunguka jua, Juma Mchopanga aliwaza mbali zaidi ya kaamua kuandika wimbo na kutuuliza kipi bora kati ya jua na mvua. Mpangilio wa mashairi ukielezea hasara na faida na kila kimoja kati ya jua na mvua naamini huu ni moja katika ya wimbo wa tofauti sana katika hili game.
MAMA KUMBENA - BANANA ZORRO
‘We mama kumbena, siamini nilichosikia.. Hutaki kumuoza binti, eti kisa umemzoea..’ haha it’s funny, inachekesha sana lakini Banana Zorro alifanya huu utunzi. Kwa jamii zetu za kiAfrika mtoto wa kike kupata mume wa kumuoa ni neema sana lakini mama Kumbena alimnyima mke Banana Zorro eti kisa amemzoea Kumbena. Siju kama ni true story au ni utunzi lakini ubunifu huu na utofauti ni ngumu kidogo kwa msanii mwingine kupata concept kama hii.
NYINGINEZO
Nyimbo zingine kwa haraka haraka ambazo naona utofauti na mawazo tofauti ambayo si rahisi kwa wasanii wengine kuimba endapo wasingeimba walioimba nyimbo hizo ni kama Usiniseme ya Alikiba, Pii Pii Ya Marlaw na Bado Nipo Nipo ya Mwana FA.
#Na Javan Watson

SASA WEMA SEPETU NA AUNTY EZEKIEL MAMBO SAFI

Hii ni picha aliyoiweka Wema Sepetu kwenye mtandao wake wa Instagram
Wawili hao wameonekana kutokuwa na tatizo baada ya madam Sepenga kuweka picha ya Aunty akiwa na mwanae Cookie aliyezaa na dansa wa Diamond, Mose Iyobo kwenye mtandao wake wa Instagram na kuandika ujumbe ambao umeonekana kutoa watu machozi.
Wema ameandika kwenye mtandao huo:
My Picture of the day…!!! This is tooo Cute…. Mola akukuuzie Cookie wako Tiake…. #Priceless 😍😍😍 Dah… Iko siku na mimi Inshallah…. Hii pic imenitoa hadi chozi…. You are sooo blessed mumy… @auntyezekiel @auntyezekiel

WCB WALIIZIDI UJANJA LEBO YA SHAA 'SK MUSIK' KUMSAINI MSANII HUYU *PICHA&VIDEO*

Label ya Shaa, SK Musik, ilizidiwa ujanja na Wasafi Records ya Diamond na kumwahi kumsainisha msanii wa huyu wa kike.
Jina lake ni Zoccu. Mwaka jana alishiriki kwenye shindano la Tecno Own The Stage lililofanyika nchini Nigeria.
Akizungumzia wasanii aliowapata kwaajili ya kuwasimamia kupitia label yake, Shaa alisema alimpata Zoccu lakini akachelewa na hatimaye kukuta mwana si wake.
“Nilimpata bwana binti mmoja anaitwa Zoccu lakini nikawa kidogo nimechelewa chelewa nikawa namuambia mwakani mara nashangaa napita Wasafi Records namkuta Zoccu kashachukuliwa,” Shaa aliiambia Millard Ayo.

Shaa amesema sasa anao wasanii wawili, Myler na mwingine kutoka Tanga na mwakani ataanza kuwatambulisha rasmi.

ANGALIA VIDEO MPYA YA AVRIL – YULE DAME

Muimbaji wa Kenya, Avril ameachia video yake mpya ya ‘Yule Dame’ iliyoongozwa na Q Bick akishiikiana na Lawdak. Tazama video hiyo hapa chini.

UMEUONA UJIO MPYA WA RAY C KIMUZIKI? *PICHAZ/VIDEO*

REHEMA Chalamila, how I wish arudi tena kwenye chati kama zamani. Ray C – kama unavyomjua zaidi, amepitia mapito mengi, na tena yaliyojaa njia yenye mbigili ibakishayo maumivu mguuni.
Miaka minne iliyopita, kwa hali aliyokuwa nayo, kila mtu alimkatia tamaa kuwa ndio basi tena ameshatumbukia kwenye shimo waliloshindwa kutoka vijana wengi. Matumizi ya madawa ya kulevya yalimuongezea jina la uteja lililolifunika jina lake la utani ‘kiuno bila mfupa.’ Rehema, msichana mrembo aliyekuwa ndoto ya wanaume wengi, akapoteza thamani yake.
Jina lake likapotea kwenye ramani ya muziki na akawa mtu wa kuonewa huruma. Na kwa jinsi madawa ya kulevya yalivyo, humnyong’onyeza mtumiaji, humpunguzia utimamu wake kiakili, humpa utegemezi unaotesa yasipotumiwa na ikawa wakati mwingi Rehema akawa wa kukutwa amezima! Maskini wa Mungu Ray C akaingia kwenye dimbwi la maji ya moto ya uteja, nani wa kumuokoa?
Kwa alama aliyoiweka kwenye muziki wa Tanzania kwa nyimbo kibao zilizofanya vizuri, Ray C akapata msaada kutoka kwa mtu mwenye cheo kikubwa zaidi nchini, Rais Jakaya Kikwete. Alijitolea kumpeleka rehab, kumsadia kwa hali na mali hadi hali yake ikarudi kwenye mstari – walau kwa muda huo. Aliingia kwenye mpango wa kutumia methadone aliodumu nao kwa takriban miaka mitatu.
Katika kipindi hicho, Ray C akageuka kuwa kinara wa vita dhidi ya matumizi ya madawa ya kulevya. Alianzisha pia taasisi yake, The Ray C Foundation kwaajili ya kampeni za kukemea ubwiaji unga. Katika kipindi hicho, Rehema, alijaribu tena kurejea kwenye muziki kwa kuachia wimbo mmoja ‘Mshum Mshum’, ambao hata hivyo haukufanikiwa kumrudisha pale alipokuwa ameishia.
Haikuwa rahisi kuishinda vita hiyo na mwaka huu alionekana kuweka silaha chini kwa kudaiwa kurejea tena kwenye matumizi ya madawa hayo. Video iliyosambaa mtandaoni akionekana akiwa kwenye mvurugano wa akili, akilia na kutaka kujichoma kisu, ilirejesha tena hofu kwa wapenzi wa muziki kuwa amerudi kwenye jela ya uteja.
RAY C ANARUDI
Peleka mbele hadi wiki moja iliyopita, Ray C anaonekana kupata chaji ya muziki inayompeleka hadi kwenye studio za kisasa za Wanene Entertainment. Kwanza nimefurahi kuona amebadilika mno kutoka yule msichana aliyenenepa hadi kuupoteza utambulisho wake. Amerudisha umbo lake la zamani linalompa matumaini ya kulikomboa jina la jukwaani – kiuno bila mfupa.
Uhakika nimeupata kwenye video alizoziweka Instagram zikimuonesha akiwa kwenye mazoezi makali ya kucheza huku kiuno chake kikifuata vyema maagizo kinayopewa. Huu unaweza kuwa urejeo wenye nguvu zaidi wa muimbaji huyu na namuomba Mungu amsaidie kukaa tena kwenye nafasi yake.
Kutoka Kushoto: Anna Peter wa East Africa Radio, Ray C na Mamy Baby wa Clouds FM
Muziki wa Tanzania unamhitaji Ray C hasa kwakuwa kuna upungufu wa wasanii wakubwa wa kike. Inanipa moyo kuona mahaba yake ya muziki yamerudi kwa kasi ya ajabu. Napata amani nikimuona anavyofurahia mchakato wa kutengeneza nyimbo mpya. Nafarijika kuona kuwa amezungukwa na watu wanaotaka arudi kwenye chati.
Atakachohitaji baada ya hapo ni kuungwa mkono na vituo vyote vya redio nchini na pia mashabiki wakitimiza wajibu wao. Yapaswa kukumbuka kuwa muziki pekee ndio unaweza kuwa mkombozi kwake na unaoweza kumpa nafasi ya pili – nafasi ya kung’ara tena.
Naamini anarekodi nyimbo nyingi na katika hizo lazima kutakuwa na nyimbo kubwa. Pamoja na matatizo yote aliyoyapita, sijawahi kuwa na shaka na kipaji chake. Nasubiri kwa hamu kusikia kile alichotuandalia.

MR BLUE ATAJA JINA ANALOTUMIA BAADA YA ‘SIMBA’ KUPOKONYWA

Rapper huyo amesema kuwa kwa sasa anatumia jina la ‘Nyani Mzee’ kama jina lake jingine la utani.
“Actually kwa sasa jina la Simba nimeliacha ila kwa sasa natumia jina la ‘Nyani Mzee’ nikimaanisha nimekwepa mshale mingi. Nasubiri na hilo wachukuwe nitafute jina jingine,” amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio.
Mwezi Disemba mwaka jana Mr Blue na Diamond waliingia kwenye mzozo kuhusiana na jina la ‘Simba’ huku kila mmoja akidai ni lake.

RAPA NYANDU TOZZY AFUNGA NDOA KIMYA KIMYA *PICHA*

Nyandu Tozzy
Msanii wa muziki wa hip hop kutoka Kundi la BOB, Nyandu Tozzy amefunga ndoa kimya kimya na mpenzi wake wa muda mrefu.
Rapa huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Kiboko ya mabishoo’ amekuwa ni msanii wa pili ndani ya mwezi huu kufunga ndoa baada ya October 15 msanii kutoka Tip Top Connection Tunda Man kuvuta jiko huko mkoani Morogoro.
Baadhi ya wasanii pamoja na wadau mbalimbali wa muziki wamepongeza msanii huyo kwa hatua aliyofikia.
nyandu-tozzy
Nyandu Tozzy na mkewe