Tuesday, May 24, 2016

ALIKIBA AWAOMBA MASHABIKI KUMPIGIA KURA DIAMOND PLATNUMZ

Sony-Alikiba
Alikiba amewaomba watanzania kumpigia kura Diamond anayewania tuzo ya BET zitakazofanyika, Juni 26 Los Angeles, Marekani.
Wiki iliyopita Diamond alitangazwa kuwania tuzo ya BET kwa mara ya pili kwenye kipengele cha Best International Act: Africa akiwa ni msanii pekee kutoka Afrika Mashariki huku tuzo hiyo ikiwaniwa na wasanii wengine kama Wizkid, Yemi Alade, AKA, Cassper Nyovest, Black Koffie, MZVEE na Serge Beynaud.
Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo, kinachoruka kupitia EA Radio, Alikiba aliwaomba watanzania wampigie kura Diamond kwenye tuzo anazoshiriki za BET na kusema kuwa yeye ndiye msanii pekee anayeiwakilisha Tanzania kwenye mashindano hayo hivyo watanzania wampigie kura ili aweze kushinda.
“Of course nawasupport wote ndiyo, vote for Diamond kwenye tuzo za BET kwa sababu yeye ndiyo anayetuwakilisha,” alisema Alikiba. 
Alikiba kwa sasa ni msanii aliye chini ya label ya Sony Music na wimbo wake mpya ‘Aje’ unafanya vizuri kwenye TV na Redio japo una siku tano tu tangu utoke, May 19.

BABY J AKANUSHA KUWA MJAMZITO

Baby J
Mwanadada anayefanya muziki wa Bongo Fleva akiwakilisha visiwa vya Zanzibar Baby J amekanusha tetesi zilizoenea kuwa ni mjamzito.
Baby J ambaye muda mwingi yupo maskani yake Zanzibar ameimbia Bongo5 kuwa ukimya wake ndiyo umesababisha watu kuhusi kuwa ni mjamzito
“Unajua kweli nimekuwa kimya lakini ni mipango naweka sawa na pia nilikuwa na mambo yangu ya kifamilia zaidi,” amesema. “Ila nashangaa watu kusema kuwa mimi ni mjamzito ni kitu ambacho kinanishangaza watu wanajua mie mjamzito wakati hata mimi mwenyewe sijui! Au kwakuwa wanaona labda nimenenepa ndio maana. Kazi zipo tayari zina subiri kutoka, kwahiyo muda wowote kazi itatoka mashabiki wake tayari tu,” ameongeza.
Hivi karibuni Mkubwa Fella alitangaza kumuongezea Baby J kwenye familia yake ya Mkubwa na Wanawe.

HAWA NDIO WATANGAZAJI WAKALI TANZANIA WANAOFANYA RAP

page
NA JOHN SIMWANZA
Watangazaji wa redio hasa vipindi vya burudani wamekua karibu sana na muziki hasa wa Hip hop /Rap na wengine kufikia hatua ya kutozizuia hisia zao ba kuamua kuingia studio na kufanya ngoma. Hata hivyo wamekuwa wanakosa sana support katika vituo vingine vya redio kucheza kazi zao. Ni wachache sana unaweza kuwasikia tofauti na vituo wanavyofanyia kazi. Hii inadhihirisha kuwa muziki wetu hapa bongo bado hauna umoja kutokana na matabaka yanayoendelea kuwepo.
page
Hawa ni watangazaji wa redio wanaofanya Rap/hip hop

SOGGY DOGGY

The entertainer ndio aka yake. Soggy ni rapa wa muda mrefu na pia ni mtangazaji wa muda mrefu na amekuwa akifanya vizuri zaidi katika muziki wa Rap na kuonekana kama wa jana vile katika game. Huyu jamaa huwa haishiwi mashairi akiamua kuitendea haki beat na ameshapita katika vituo kadhaa vya redio kama mtangazaji zikiwemo Uhuru FM, Radio Free Africa, Triple A, EFM, Ebony FM na Mashujaa FM. Soggy ni miongoni mwa malegend wa muziki huu Tanzania. Soggy ana orodha nyingi zaidi ya nyimbo alizowahi kufanya kuliko mtangazaji mwingine zikiwemo Kibanda cha Simu, Nafunga Zipu, Zai, Kulwa na Dotto na zingine kibao.
SAIGON 
Hapana shaka juu ya mwana hip hop huyu wa muda mrefu na mwanzilishi wa kipindi cha Hip Hop Base kilichokuwa kinaruka katika runinga ya Channel 5 zamani na sasa inajulikana kama EATV.
Saigon ni msanii mwenye flow kali sana na yuko tofauti na wasanii wengine wa rap hapa nchini. Pia Saigon ni fundi wa kuhost live show na huwa anateka mashabiki. Tumeona hata katika mashindano ya Dance 100% ambapo amechangia kwa kiasi kikubwa shindano hilo kupendwa zaidi. Rapper huyu ana ngoma kadhaa ambazo ameshafanya zikiwemo Poverty, Soma, Kibongobongo, Rudia na zingine.


BAGHDAD 

Mexcana Lacavela ndio kundi lililomtambulisha kwenye game ya muziki wa hip hop na kituo cha Clouds FM ndicho kilichomtambilisha katika fani ya utangazaji. Hitmaker huyu wa Haters, ni msanii mwenye tungo kali sana na ukimsikiliza kwa makini utagundua hili.
Amepita katika vituo kadhaa vya redio ikiwemo Clouds FM, EFM, na sasa yupo TBC FM kwenye kipindi cha Papaso .

PHILBERT KABAGO 
Ni msanii anayeipeperusha bendera ya Mwanza. Japo sio maarufu sana ila kwa wafuatiliaji wa muziki kiundani na wapenzi wa redio mbalimbali jina hili la Kabago sio geni. Aliwahi kufanya vizuri na kundi la BWV la Mwanza. Jamaa alikuwa mtangazaji wa Passion FM kabla ya kuhamia Lake FM. Anajihusisha sana na muziki wa rap hasa katika kutetea jamii.
Ameshazungumzia mambo ya miundo mbinu mibovu ya jijini Mwanza kwa wimbo wa ‘Barabara.’ Ngoma zake zingine ni pamoja na Hakuna Kuremba na Umeme wa Mgao.

ADAM MCHOMVU
Ni zao asilia kabisa la muziki wa hip hop na hawezi kukushangaza kufanya hip hop kwani anakotoka Arusha ambako ndiko kuna nembo na chembechembe za muziki huu wa hip hop hapa Tanzania. Mchomvu ni mtangazaji wa Clouds FM na anafanya vizuri sana katika taaluma yake na amekuwa akisupport sana hip hop muda wote. Adam Mchomvu ameshafanya ngoma kadhaa ikiwemo Tiririka, Bwana Shamba,Johnyyy,Aisha,Aeiou na zingine nyingi zinazompa heshima katika list ya hawa watangazaji wanaorap.
SKYWALKER 
Fredrick Bundala ndio jina analotumia kwenye serious issues. Ni ni songwriter,producer,mchambuzi wa masuala ya burudani, mwandishi wa vitabu na mtangazaji. Na kubwa zaidi huyu ni rapa mkali sana na ana ngoma nyingi alizowahi kufanya zikiwemo, Nimesota, Mawili Matatu, Ujana Be Your Man na zingine.
Skuwizzy anaingia katika list hii kwa kukidhi sifa zote kwa wanaofuatilia Radio Free Africa. Miaka ya 2007 watakubaliana na mimi kuwa miongoni mwa vipindi vizuri katika radio, vyake vilikuwa vinaingia vyote ikiwemo Extra Showtime, RFA Music Chat Show pamoja na Sitosahau. Hivi karibuni alitoa album ya beat alizoziandaa na kubwa zaidi Skywalker ni msanii wa kwanza kufanya cover ya wimbo wa Dr Dre, Talking to My Diary uliopo kwenye album ya Compton.
SAM MISAGO
Ni moja kati ya watangazaji tegemezi Tanzania. Amekuwa akifanya vipindi vya burudani tangu tulipomfahamu na hajawawahi kupwaya katika vipindi alivyowahi kufanya na anavyoendelea kufanya. Misago amedhihirisha kuwa yeye sio tu mpenzi wa Rap pia ana uwezo wa kufanya Rap. Ana ngoma mbili mpaka sasa ambazo ni Ballin and Chillin na Nimepania.

EZDEN 

The Rocker ndio aka ya huyu jamaa mbunifu wa kupitiliza. Ezden ndio muanzilishi wa kipindi hiki cha Kiss Collabo Mix katika kituo cha Kiss FM kilichopo chini ya kampuni ya Sahara Media Group.
Ezden mbali na kufanya vipindi vya burudani pia ni rapa na freestyler mzuri sana anayeweza kunata na beat yoyote.