Monday, August 31, 2015

SHUHUDIA MKUTANO WA KAMPENI DUNI HAJI MGOMBEA MWENZA CHADEMA HUKO MTWARA


Mgombea Mwenza CHADEMA+UKAWA Juma Duni Haji akiwahutubia mamia ya wakazi wa Mtwara kwenye kampeni Jana



MAMA MZAZI WA ZARI ATEMBELEA ‘IKULU’ YA DIAMOND PLATNUMZ *PICHAZ*


Zarimond
Mtoto Latiffah Nassib a.k.a Princess Tiffah anazidi kuongeza ukaribu kati ya familia za wazazi wake, Diamond pamoja na Zari.
Takribani wiki tatu baada ya Zari kujifungua, mama yake mzazi amefunga safari kuja Tanzania kumsalimia binti yake pamoja na kumuona mjukuu wake.
mama zari
Mama yake Zari akiwa amembeba Tiffah
Zari ameshare picha ya mama yake akiwa amemtambelea nyumbani kwa Diamond akiwa amembeba Tiffah na kuandika;
“Good morning, tag someone your blessed to have in your life. Here is my mom and my daughter”

MH.PAUL MAKONDA KATIKA UZINDUZI WA VITABU VYA MWL.LILIAN NDEGI

Mh.Paul Makonda akizindua vitabu 
Mh.Paul Makonda alipokuwa akionesha vitabu baada ya kuzindua
Mkuu wa Wilaya Kinondoni Mh.Paul Makonda siku ya jana katika kanisa la Living Water Center chini ya mtumishi wa Mungu Apostle Onesmo Ndegi alikuwa mgeni wa heshima katika uzinduzi wa vitabu vitatu  "MJUE MWANAMKE,USIIPE HOFU NAFASI na RAFIKI ANAYEKUFAA vilivyoandikwa na Mwl Lilian Ndegi wa Kanisa la Living Water Center Kawe.

Ibada hiyo ya uzinduzi wa vitabu ilipambwa na vikundi vya uimbaji sifa kama Living Waters wenyeji Upendo Nkone,GUG Dancers na More Than Enough Band.

Mkuu huyo wa wilaya ndiye aliyezindua vitabu hivyo na kuendesha zoezi zima la uuzaji wa vitabu hvyo,kwa kuanza alinunua vitabu hivyo vitatu kwa shiling Milioni 5 ikiwa ni kuchangia na kusapoti huduma hiyo ya uandishi wa vitabu vya Mwl Lilian Ndegi ambaye ni Mama yake kwa malezi ya kiroho kanisani hapo Living Water Center Kawe.

Katika uzinduzi huo uliambatana na kukata keki ikiwa ni ishara ya kufurahia mafanikio ya kazi ya uandishi wa Mwl Lilian Ndegi na ugawaji wa zawadi katika tukio hilo ulifanyika kwa watu ambao wamekuwa wakihusika katika ufanikishaji kwa namna moja au nyingine au kumuwezesha Mwl Lilian kufanikisha uandishi wake wa vitabu.

Mh Paul Makonda aliwasihi washirika wa Kanisa la Living Water Center Kawe kusapoti kazi ya Mwl Lilian ikiwa ni kwa kununua na kuvisambaza vitabu vyake ili viwafikie wasomaji wengi ikiwa vitaleta matokeo mazuri katika maisha yao kutokana na ujumbe ulio ndani ya vitabu hivyo.

Apostle Onesmo Ndegi kiongozi wa Kanisa la Living Water Center na mme wa mwandishi wa vitabu Mwl Lilian Ndegi katika kuzungumza kwake alikuwa akijivunia Mkuu huyo wa Wilaya na kusema ni kijana wake anamfahamu vizuri siku nyingi tangu bado anasoma na kusema amelelewa hapo na kusema kuwa alikuwa msikivu,na mpaka Mh Rais kumteua kwa nafasi hiyo ya kuwa Kiongozi wa Wilaya hakukosea.
Apostle Ndegi akimlisha keki Mwl Lilian Ndegi ambaye ni mke wake ikiwa ni ishara ya kupongezana
Mh.Paul Makonda akilishwa keki Mwl Lilian Ndegi mwandishi wa vitabu vilivyozinduliwa
Baadhi ya wageni waliokuwa wamealikwa katika uzinduzi huo wa vitabu wa kwanza kush Mchungaji Deborah Ntepa,Mama Mchungaji Tumwidike koka Mbeya na Mwl. Lilian ndegi mwenyeji
Mh.Paul Makonda alipokuwa akiwakabidhi vitabu baadhi ya watu walionunua baada ya kuvizindua
Mh.Paul Makonda alipokuwa akiwakabidhi Mzee wa Kanisa vitabu baadhi ya watu walionunua baada ya kuvizindua
Mh.Paul Makonda alipokuwa akiwakabidhi Kiongozi wa mabinti Kanisani hapo Magreth vitabu baada ya kuvizindua

Mama Mchungaji Tumwidike kutoka mbeya alikuwepo katika uzinduzi huo
Mchungaji Deborah Ntepa kutoka Oasis Healing Ministry alikuwepo katika uzinduzi huo
Upendo Nkone alipokuwa akihudumu katika ibada ya uzinduzi wa vitabu iliyoongozwa na Mh. Makonda

Mwl Lilian Ndegi na Upendo Nkone wakicheza mbele za Bwana ilikuwa full shangwe
Mh.Paul Makonda wa kwanza kushoto,katikati ni Apostle Ndegi Kiongozi wa Kanisa la Living Water Center na wa mwisho ni Mwandishi wa vitabu Mwl. Lilian Ndegi 
Mh.Paul Makonda na Mwandishi wa vitabu Mwl. Lilian Ndegi katika picha ya pamoja baadhi ya mabinti  wa kanisani hapo.
Mwandishi wa vitabu Mwl. Lilian Ndegi katika picha ya pamoja baadhi ya wakina mama wa  kanisani hapo.

CCM JIMBO LA KAWE YAZINDUA KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU YAMNADI KIPPI WARIOBA

Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba (katikati mbele), akisindikizwa na wanachama wa chama hicho, alipowasili katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati CCM ilipozindua kampeni kwaajili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, katika jimbo hilo, jijini Dar es Salaam jana.
PICHA/JOHN BADI WA DAILY MITIKASI BLOG
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge (kulia) akimtambulisha Mgombea Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya CCM, Kippi Warioba mbele ya umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi wa kampeni kwaajili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, katika jimbo hilo, jijini Dar es Salaam jana.
Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba ‘Gadafi’ (kulia) akimpongeza Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya CCM, Kippi Warioba baada ya kumkabidhi Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015, mbele ya umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi wa kampeni jimboni humo, jijini Dar es Salaam jana.
Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba ‘Gadafi’ (kushoto) akimtambulisha Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya CCM, Kippi Warioba baada ya kumkadhi Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015, mbele ya umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi wa kampeni jimboni humo, jijini Dar es Salaam jana.
Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba (kulia), akiusalimia umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, baada ya kutambulishwa na kukabidhiwa Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015, wakati wa uzinduzi wa kampeni jimboni humo, jijini Dar es Salaam jana. Kulia kwake ni Katibu Mwenezi wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba ‘Gadafi’.
Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba akizungumza umati wa wanachama wa CCM na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi wa kampeni kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, katika jimbo hilo, jijini Dar es Salaam jana.
Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba akiinadi Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015, mbele ya umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi wa kampeni jimboni humo, jijini Dar es Salaam jana.
MAMA MZAA CHEMA … Mama Evelyne Warioba ambaye ni mama mzazi wa Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba akiusalimia umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi huo. 
Sehemu ya umati wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi huo. 
Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Salum Londa akimwaga sera za CCM mbele ya umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi huo. 
Mhamasishaji maarufu kwa jina la ‘Msaga Sumu’ naye alikuwepo.

CHADEMA YATOA ILANI YAKE KATIKA MOSHI


Meneja Kampeni wa mgombea Ubunge katika jimbo la Moshi mjini kupitia Chadema na UKAWA,Jafary Michael ,Bw Raymond Mboya akifanya utamburisho mbele ya wanahabari wa mkutano wa mgombea huyo na wanahabari uliofanyika katika Hotel ya Keys.X
Waandishi wa Habari mkoa wa Kilimanjaro ambao ni wawakilishi wa vyombo mbalimbali vya Habari nchini wakiwa katika kikao na mgombea Ubunge jimbo la Moshi mjini kupitia Chadema na UKAWA,Jafary Michael.
Mbunge wa jimbo la Moshi mjini aliyemaliza muda wake ,Philemoni Ndesamburo(Chadema) akizungumza na wanahabari (hawako pichani) wakati wa kikao cha mgombea Ubunge wa jimbo hilo kueleza Ilani ya chama chake katika ngazi ya jimbo hilo.
Baadhi ya wanahabari.
Mgombea Ubunge katika jimbo la Moshi mjini,Jafary Michael akizungumza katika kikao hicho kuelezea kilchomo katika ilani ya Chadema ngazi ya jimbo la Moshi mjini.
Baadhi ya wanahabari.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii
ILANI YA CHADEMA KATIKA MANISPAA YA MOSHI.
1.      ELIMU:
A.     ELIMU YA AWALI:
·         Kuimarisha madarasa ya awali.
·         Upatikanaji wa walimu wa awali.

B.      ELIMU YA MSINGI:
(i)                 Kuongeza matundu ya vyoo katika shule za msingi ndani ya Manispaa ya Moshi.
(ii)               Kujenga silos katika shule mbalimbali za msingi ya kuhifadhi nafaka za shule.
(iii)             Kuongeza nyumba za walimu.
(iv)              Kuongeza madarasa na kukarabati  yaliyopo.
(v)                Kusaidia kulipia michango ya chakula kwa watoto yatima na wanaotoka familia duni
(vi)              Kuimarisha elimu ya computer katika shule zetu za msingi.
(vii)            Kuongeza mtandao wa maji safi kwa shule za msingi.

C.      ELIMU YA SEKONDARI:
·         Kuongeza matundu ya vyoo
·         Kuongeza na kuimarisha miundombinu ya vyumba vya maabara.
·         Kuongeza vyumba vya kulia chakula (mabwalo).
·         Kujenga maktaba katika shule za sekondari.
·         Kupandisha daraji baadhi ya shule za kawaida kuwa za kidato cha tano na sita.
·         Kuhakikisha familia duni na za watoto yatima zinasaidiwa michango mbalimbali ya shule.


(2) AFYA:
·         Kusukuma upatikanaji wa hospitali ya Wilaya.
·         Kuimarisha vyumba vya upasuaji katika vituo vya afya.
·         Kuboresha zahanati.
·         Kujenga vyumba vya kuhifadhia maiti katika vituo vya afya.
·         Kujenga uzio katika vituo vya afya na zahanati ili kudhibiti usalama wa wagonjwa.
·         Kusukuma kusimamia kwa sera ya matibabu ya bure kwa wazee na watoto chini ya miaka mitano.
·         Kuongeza na kuimarisha vyumba vya kuzalishia. (labour ward)
·         Kuongeza nyumba za waganga wa vituo.

(3) MAJI:
·         Kuongeza mtandao wa maji safi na maji taka kwa kushirikiana na mamlaka ya maji safi na maji taka.((MUWSA)
·         Mh: Kata ya Kiboriloni, Longuo B na Rau.

(4) Makundi maalum:
·         Kuboresha miundombinu ya makundi maalum katika majengo ya serikali
·         Kuimarisha na kuboresha miundo mbinu ya shule za watu wa makundi maalum.
·         Kushirikiana na vyama vya watu wenye ulemavu
·         Kushirikiana na Asasi za kiraia zinazohudumia makundi maalum katika jamii

(5) MIUNDO MBINU:
·         Kuongeza mtandao wa barabara za lami kwenye maeneo ya katikati ya mji na
Kata za pembezoni.
·         Kupandisha barabara za kiwango cha vumbi kwenda kiwango cha changarawe(moramu)
·         Kuimarisha barabara mbalimbali ndani ya Kata na Mitaa yake katika manispaa ya Moshi.
·         Kujenga na kuimarisha mfereji wa maji ya mvua katika manispaa ya Moshi ili kulinda barabara za Manispaa.
·         Kujenga vivuko na kumalizia madaraja ndani ya Manispaa ya Moshi.
·         Kuongeza na kuimarisha mtandao wa taa za barabarani.

 (6) UCHUMI:
(A) AJIRA:
(i) Tutaendelea kuboresha ajira zisizo rasmi (informal sector) ili ziwezeshwe kurasimishwa.
·         Kutenga maeneo rasmi
·         Kuzuia matumizi nguvu kwa wajasiriamali wakiwepo wamachinga wadogo.
·         Kuwapa elimu
·         Kuwathamini wafanyabiashara sekta muhimu katika kukuza uchumi wa Moshi.

(ii) Kuendelea kuviwezesha vikundi vya vijana na kinamama kwa kutumia fedha za mfuko wa  vijana na kina mama.


(iv) Kuendelea kuhamasisha uanzishwaji wa vikundi vya vikoba na saccos na kuimarisha       vilivyopo.

(v) Kuendelea kusukuma Serikali Kuu ili kufufua viwanda vilivyo binafsishwa kwa ajili ya kutoa ajira kwa wananchi wa Moshi na mkoa wa Kilimanjaro kwa ujumla.

(vii) Kuendelea kujenga mazingira rafiki na mahusiano mazuri na sekta binafsi ili kusukuma na kuharakisha uwekezaji katika mji wa Moshi kwa ajili ya kuongeza ajira. (Service levy)

(viii) Kulinda na kusimamia matumizi sahihi ya rasilmali za halmashauri ikiwepo kutafuta wawekezaji katika maeneo ya Halmashauri ya Manispaa ya Moshi.

(xi)  Kuendelea kuongeza mapato ya Halmashauri mwaka hadi mwaka kwa kuboresha mfumo wa takwimu za ukusanyaji wa mapato. (Data base)
(B)UTALII:
(i) Kuangalia uwezekano wa kuongeza vivutio vya watalii katika Manispaa ya Moshi ikiwepo kuendeleza mazungumzo na Wizara ya Mali Asili na Utalii ya kuingia ubia na Manispaa ya Moshi ya kuboresha msitu RAU.

(ii)  Kuhamasisha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuwekeza katika hoteli za kitalii za nyota tatu mpaka tano ili kuongeza idadi ya watalii wanaolala katika mji wa Moshi.

(iii) Kuendelea kusukuma uboreshaji wa uwanja wa ndege wa Moshi (Moshi Airport) uweze kufanya kazi kwa ufanisi .

(iv) Tutaendelea kutetea maslahi ya wapagazi na kushirikiana na vyama vyao.

(C) MCHAKATO WA MANISPAA YA MOSHI KUWA JIJI LA MOSHI.
Kuendelea kumshawishi Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atoe tamko la Moshi kuwa jiji baada ya kukamilisha mchakato wote kwa mujibu wa sheria.

(D)KILIMO:
 kuendelea kuboresha kilimo cha mjini (Urban agriculture) kwa kuimarisha kilimo cha kisasa katika ukanda wetu wa kilimo ndani ya Manispaa ya Moshi ikiwa ni pamoja na uvuvi na ufugaji.

(E) MASOKO:
 Kusimamia uboreshaji masoko ya manispaa ili yafanye kazi kwa ufanisi.

(7) MICHEZO:
(a) Kuendelea kuimarisha viwanja vya michezo katika Manispaa ya Moshi.

(b)  Kuimarisha ushindani wa wanamichezo katika Kata za manispaa ya Moshi ili kuibua vipaji mbalimbali katika michezo ya aina tofauti.

(c) Kuhamasisha wadau mbalimbali kuchangia timu za michezo tofauti katika Manispaa ya Moshi ili kupata timu za michezo mbalimbali zitakazowakilisha manispaa katika michezo ya kitaifa.

(d) Halmashauri ya Manispaa ya Moshi itaandaa sera za michezo inayooanisha michezo na uchumi na michezo na ajira ili kuondoa dhana kuwa michezo ni burudani tu.

(8) MAZINGIRA:
(a) Kuhamasisha upandaji wa miti katika maeneo mbalimbali ya Manispaa.

(b) Kutunza vyanzo vya maji.

(c) Kuendeleza usafi wa mji wa Moshi;

 (i)Kutoa elimu kwa wananchi wa Moshi

 (ii) Kuhamasisha watu kutenga takataka katika vyanzo (separation at source)
(iii) Kufanya takataka kuwa rasilimali na sio uchafu hivyo kuzalisha ajira.
(iv) Kutengeneza gesi asilia (Bio gas) na  mbolea ya mboji
(v)  Kuongeza vitendea kazi kama magari na vinginevyo.
(vi) Uboreshaji wa dampo kuu (land field).

(9) ARDHI NA MIPANGO MIJI:
(a) Upimaji wa maeneo ya makazi kwa kuondoa ujenzi holela.

(b) Kupima maeneo ya halmashauri ya manispaa ya Moshi  kwa ajili ya kupata hatimiliki.

(c) Kusimamia ujenzi unaoendelea na mpango kabambe wa uendelezaji wa mji wa Moshi (Master plan) ya mwaka 2001)

(d) Kuzuia uvamizi wa maeneo ya wazi

(e) Kutengeneza na kusimamia mpango kabambe wa miaka kumi na tano wa kuendeleza mji wa Moshi, utahusisha Kata za Majengo, Bomambuzi, Korongoni, Kiusa,Mawenzi na Bondeni.

(f) Kukabiliana na migogoro ya ardhi inayosababishwa na idara ya ardhi ikiwepo kugawa kiwanja kimoja zaidi ya mtu mmoja.

(g) Kusukuma upatikanaji wa hati miliki kwa wakati.
 MWISHO .

WAKILI MAARUFU PETER KIBATALA AELEZA MANTIKI YA LOWASSA KUWATOA MASHEIKS & BABU SEYA

Babu Seya na Mwanawe Wakiwa Chini ya Ulinzi wa Magereza
Kuna watu wanajaribu kupotosha nini hasa mantiki ya Mgombea Edward Lowassa kuahidi kushughulikia suala la Sheikhs wa Zanzibar na suala la Babu Seya.
Suala la Sheikhs wa Zanzibar liliihusisha Chadema kabla hata Lowassa hajahamia huku. Binafsi niliombwa na Dr Slaa kulishughulikia, lakini bahati mbaya nilikuwa nina cases kadhaa zilizonifanya nikwame. Lakini cha muhimu zaidi ni kwamba wana Wakili, tena Wakili mahiri tu na ambaye ni Mwanachama wa Chadema. Amepambana sana, na anaendelea mpaka leo.

Issue yao ni complicated, na ni mfano tu wa issues zinazo athiri haki za wananchi kwa kukosekana tu utashi sahihi wa kisheria na kiutawala.
Mojawapo wa pertinent issues ni mgogoro wa iwapo wanatakiwa kishtakiwa Bara, au Zanzibar inakosemekana walitenda huo ugaidi. 
Na kuna masuala ya Sheiks wale kulalamika kutendewa kinyume wakiwa chini ya ulinzi. 
Kuna suala pia la ucheleweshaji wa upelelezi, hata kama tuna-assume case dhidi yao ina mashiko.
Asiyefahamu anaweza kudharau uzito wake, lakini ni suala linaloleta hisia kali kwa sehemu ya waumini wa kiislamu. 
Lowassa atakuwa Rais wa ajabu kama vision yake ya kisheria haitajumuisha suala pertinent kama hilo. Huwezi jadili general concepts bila kuchagua specifics kadhaa kama mfano. 
Pia, Lowassa hajasema atamtoa Babu Seya kwa stroke ya pen on a whim. Wala hajasema hiyo ni priority yake above all else kwa upande wa sheria. Alichosema within the limited confines za muda ni kwamba serikali yake itakuwa makini sana na masuala ya utawala wa sheria. Issue ya Babu Seya na hao Sheiks ni representation tu ya matatizo yaliyopo. Na malalamiko yaliyopo. Issue ya Lawrence Masha na wale vijana 19 wa 4U Movement tuliowapigania juzi, imepigia mstari.
Pamoja na kwamba ni suala linalogawa opinion, ni naivety kujidai eti issue ya Babu Seya si moja ya issues zinazoleta mjadala wa kisheria na kihisia mpaka leo hii. Suala la ni namna gani linashughulikiwa, ni suala la ushauri wa kisheria kutoka kwa wataalamu wa Rais Lowassa (kipindi hicho).