NYOTA wa timu ya Olympique Marseile ya ligi ya Ufaransa Dimitri Payet amemzidi kiungo wa Chelsea katika orodha ya wachezaji waliotengeneza nafasi nyingi za wenzao kufunga mabao katika ligi 5 bora barani ulaya .
Tangu Cesc Fabregas ajiunge na Chelsea akitokea Barcelona mwanzoni mwa msimu huu ameweza kuwa kinara wa kutengeneza mabao kwa wenzie akiwa ametoa pasi za mwisho mara 14 idadi inayomfanya kuwa mchezaji anayeongoza katika takwimu hiyo kwenye ligi ya England .
Hata hivyo Payet ametengeneza nafasi nyingi zaidi uliko Fabregas huku tofauti kubwa kati ya wawili hawa ikiwa jinsi ambavyo wachezaji wa Chelsea wameweza kuzitumia vizuri pasi za Fabregas kufunga tofauti na wachezaji wa Marseile.
Orodha ya wachezaji waliotengeneza nafasi nyingi barani ulaya hadi hatua hii ya msimu inaongozwa na Dimitri Payet huku akifuatiwa na Fabregas na nafasi ya tatu inashikwa na kiungo Mbelgiji Kevin De Bruyne ambaye ametengeneza nafasi 59 huku akiwa anaongoza kwenye ligi ya Ujerumani.
Dimitri Payet anaongoza kwa kutengeneza nafasi nyingi za kufunga kwenye ligi tano bora barani Ulaya.
Orodha hii imejaa wachezaji toka kwenye ligi ya England ambapo Stewart Downing wa West ham United anashika nafasi ya nne akiwa ametengeneza nafasi 54 ambapo anafuatiwa na Dusan Tadic wa Southampton ambaye ametengeneza nafasi 53 huku Alexis Sanchez wa Arsenal na Eden Hazard wa Chelsea wakiwa wamefungana kwenye nafasi ya sita baada ya kutengeneza nafasi 53 kwa kila mmoja .
Mchezaji wa Liverpool Raheem Sterling ambaye ametengeneza nafasi 49 naye ameingia kwenye orodha hii akiwa kwenye nafasi ya 7 , mbele ya kiungo mshambuliaji wa Swansea Gylffi Sigurdson ambaye anashika nafasi ya 8.
Orodha hii ya wachezaji wanaoongoza kwa kutengeneza nafasi kwa wenzao kufunga imejumuisha wachezaji wengine kama Christian Eriksen wa Tottenham na Jesus Navas wa Manchester City pamoja na Santi Cazorla wa Arsenal ambapo Eriksen ametengeneza nafasi 46 huku Cazorla na Navas ambao wote ni raia wa Hispania wakiwa wametengeneza nafasi 45.
Eden Hazard ni moja kati ya wachezaji walio kwenye orodha ya wachezaji 10 kwa kutengeneza nafasi nyingi za kufunga barani ulaya.
Mchezaji wa Werder Bremen Zlatko Junuzovic ameshina nafasi ya 11 baada ya kutengeneza nafasi za kufunga 43 na nyuma yake wako Lionel Messi wa Barcelona na Leighton Baines wa Everton ambao wametengeneza nafasi 42 za kufunga
Mchezaji anayepewa nafasi kubwa ya kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia Cristiano Ronaldo ametengeneza nafasi 39 huku orodha hii ikionyesha kuwa Ligi ya England ,Ujerumani na Ufaransa zinaongoza kwa kutengeneza nafasi nyingi za kufunga mbele ya ligi ya Hispania huku kukiwa hakuna mchezaji wa ligi ya Serie A kwenye orodha hii.
0 comments:
Post a Comment