USAJILI
wa kiungo Arturo Vidal kutoka Juventus kwenda Manchester United umepata
ganzi kufuatia mashaka ya kutokuwa fiti kwa nyota huyo wa Chile, hii ni
kwa mujibu wa kocha wake wa timu ya taifa.Kocha
wa Chile Jorge Sampaoli ameliambia gazeti la El Mercurio la nchini humo
kuwa bosi wa United, Louis van Gaal anahofia kutumia pauni milioni 47
kwa Arturo Vidal ambaye aliandamwa na maumivu ya goti.
Vidal
amekuwa akiwindwa na United na kwa muda mrefu ambapo katika muda wote
wa dirisha la usajili la kiangazi, usajili wake wa kwenda Old Trafford
umekuwa ukionekana uko jirani.
“Najua
tatizo kubwa la usajili wake wa pauni milioni 47 kwenda Manchester
United ni Van Gaal kuwa na mashaka na maendeleo ya goti la Vidal,”
alisema kocha Jorge Sampaoli.
Kocha
huyo wa Chile raia wa Argentina, alisema ana uhakika Vidal alionyesha
kiwango cha asilimia 30 au 40 tu katika michuano ya kombe la dunia
kulinganisha na ubora wake uliozoeleka Juventus.
0 comments:
Post a Comment