Monday, March 31, 2014

WAZIRI MKUU PINDA AMKABIDHI TUZO YA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14


Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kushoto) akimvisha medali ya Mwanamke Bora wa Mwaka 2013/2014, Dk. Maria Kamm.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni tano Dk. Maria Kamm aliyetwaa Tuzo ya Mwanamke Bora wa Mwaka 2013/2014 ndani ya Ukumbi wa African Dreams uliopo Area D, Dodoma
Waziri Mkuu akimkabidhi tuzo, Anna Margareth Abdallah, kwa niaba ya mshindi wa pili ambaye ni Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro.
Waziri Mkuu akimkabidhi tuzo Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Profesa Anna Tibaijuka aliyeibuka mshindi wa tatu katika tuzo hizo.
Mbunge wa Same Mashariki (CCM), Anne Kilango Malecela, akipokea tuzo kutoka kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda baada ya kushika nafasi ya nne.
Dk. Maria Kamm akipokea tuzo kutoka kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda baada ya kuibuka kinara wa Tuzo ya Mwanamke Bora wa Mwaka 2013/14.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (katikati) katika picha ya pamoja na washindi walioingia Nne Bora. Kutoka kushoto; Anna Abdallah aliyechukuwa tuzo kwa niaba ya Dk. Asha-Rose Migiro, Anne Kilango Malecela, Dk. Maria Kamm na Profesa Anna Tibaijuka.
Mkuu akiwa katika picha ya pamoja na washindi, waandaaji wa tuzo hizo kutoka Global Publishers Ltd.
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers & General Enterprises Ltd, Eric Shigongo, akitoa hotuba fupi wakati wa utoaji tuzo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi ambaye alikuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Mgeni rasmi, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akihutubia kabla ya kukabidhi tuzo.

Dk. Maria Kamm na mumewe wakifuatilia hotuba ya Waziri Mkuu Pinda.
Anne Kilango Malecela na mumewe Mzee John Samuel Malecela wakiwa katika hafla hiyo.

Wageni waalikwa wakiimba Wimbo wa Taifa.
Mama Magreth Sitta (katikati) na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Ester Bulaya (kulia) wakifuatilia zoezi la utoaji tuzo.

Dk. Kamm na mumewe wakiangalia Tuzo ya Mwanamke Bora wa Mwaka 2013/14.
Shigongo na Waziri Mkuu wakiteta jambo.
Profesa Tibaijuka akisalimiana na Mama Anne Kilango.
Dk. Kamm akisakata rhumba na Profesa Tibaijuka.
Waziri Mkuu akiongea jambo na mume wa Dk. Kamm. Kushoto ni Dk. Maria Kamm.

UZINDUZI WA TV 1 ULIVYOFANA, BURUDANI KABAMBE TOKA KWA NAVY KENZO NA BARNABAS

TV 1 imekuwa ni runinga inayoshika kasi sana hapa mjini kitu kinachotishia hata uwepo wa wale wakongwe hapa mjini, mwishoni mwa mwezi uliopita televisheni hii mpya na maarufu hapa mjini kwa kuonyesha movies na vipindi kabambe vya burudani lakini pia ikiwa ni tv inayokuja vizuri katika uwanda wa habari, ilifanya uzinduzi wake ambao ulifanyika katika hoteli ya Southern Sun ambapo waliitisha mkutano na waandishi wa habari na kueleza mengi ikiwemo mambo ambayo kama luninga mpya wamejiandaa kuwaletea watanzania kupitia kituo chao kinachorusha matangazo yake kutokea jijini Dar es salaam na kuonekana nchi nzima.

Siku si nyingi wanafamilia hawa wa Tv 1 waliamua kufanya sherehe ili kusherehekea ujio wao mpya na wa kuvutia na uliokubalika na mioyo kunjufu ya watanzania, ambapo party hii ya kuvutia ilifanyika katika ukumbi wa The Terrase uliopo Slipway.

Wageni lukuki walialikwa katika sherehe hii ambayo ilitumbuizwa na wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya almaarufu kama bongoflava, ambapo wasanii wa kundi la Navy Kenzo, Aika na Nahreel walitoa burudani ya kutoka kwa wageni waalikwa, lakini pia mzee wa masauti Barnaba Classic au waweza muita baba Steve nae alikuwepo na kufanya yake.
Mkurugenzi mtendaji wa Tv 1 Tanzania, Bw. Marcus Adolfsson akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa The Terrase uliopo Slipway, mwishoni mwa wiki iliyopita wakati wakisherekea kuanzishwa kwa kituo hicho bora cha burudani


Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Bw. Godfrey Simbeye akiongea na waandishi wa habari juu ya ujio huu mpya wa TV 1 katika hafla hiyo iliyofanyika ukumbi wa ‘The Terrace Slipway’, Jijini Dar es salaam.
Burudani na Barnabas, ambaye aliimba vibao vyake matata vilivyokonga nyoyo za waliohudhuria katika uzinduzi huo
Mwanamuziki Angel pia hakuwa mbali na uwanja wa burudani ambapo alipanda jukwaani na Barnaba kusherehesha
Navy Kenzo nao hawakuweza kuwaacha wapenzi wao wa wimbo mzuri wa 'Chelewa' wapitwe na mambo, nao wakafanya yao.

Watu wakacheza muziki na kunywa huku mambo mengine yakiendelea, Check hawa wanavyoyarudi magoma
Haya sasa tucheze 'Bhokodo'….
Kila mtu aka show love kwa waimbaji..
Kemi Kaalikawe na Jokate Mwegilo wakifurahia burudani toka kwa wasanii.
Baada tu ya wasanii kushuka toka jukwaani hawa jamaa walilivamia jukwaa na kuanza yao

Huku wengine wakiendelea kutokelezea jukwaani, wengine wakaanza mapozi ya picha..
Haya sasa pozi na wadau
Tumetokelezea eeeeeeeh!!!!




Innocent Msuha (Kushoto) na Mukhsin Mambo (kulia) toka TV 1 Habari ambapo Bw. Mukhsin ndiye Mhariri mkuu katika dawati la habari.

Jina lake muite Angel, mwanadada mwenye masauti aliyeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Tusker Project Fame, kwa sasa yupo kama solo artist akitamba na kibao chake cha 'Nisamehe' na pia ni mmoja wa team ya TV One  kama muandaaji wa kipindi cha 'The one show'
na siku hiyo alimpa sapoti Barnaba Elias.
Martin Kadinda na Jokate Mwegelo ambaye ni mtangazaji wa kipindi cha 'The one show'
WanaTv 1 wakiwa na nyuso za kutabasamu wakiashilia mwanzo mzuri!
C.O.O wa MTG Afrika Bw. Rune Skogeng (aliyevaa suti) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa TV 1 Tanzania, Bi. Irene Stanley (Wa kwanza kushoto), Eugenia Chanda (katikati) na Chantelle Asante (Wapili toka kwa Rune) kwenye party hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa The Terrace uliopo Slip way
Jokate na Andre Mahiga
Borah, Angel, Lulu


Linda na Bonaventura
Mapacha nao walikuwepo..!
Mbando wa Airtel (kulia) nae alikuwepo
Oz Sinare (kushoto)  na Bw. Evance Bukuku
Kulia kabisa ni Emanuel Chriss vocalist mmoja hatari sana, akiwa na Mkurugenzi mtendaji wa TV 1 Tanzania Bw. Marcus Adolfsson na baadhi wadau wakubwa wa TV 1.
Dj nae hakuwa nyuma, akaweka pozi kupigwa picha.
Nguo aliyovaa Jokate ilikuwa matata sana, kama ada picha ikachukliwa, ila mmmmh alitokelezeaaa... 








 








Picha na Frank Mavura, Mukhsin Mambo na Bongo5blog