MAHAKAMA moja nchini Misri imempa mwanablogu mmoja kifungo cha miaka mitatu gerezani kwa kukufuru na kudharau dini.
Alber Saber alikamatwa mwezi wa tisa baada
ya majirani kumlaumu kwama ndiye aliweka
kilinganishi cha mtandao kilichoashiria sinema iliyoidhihaki dini ya
Kiisilamu, na iliyosababisha maadamano makali katika ulimwengu wa
Kiislamu.
Bwana Saber, ambaye haamini Mungu
yeyote na anayetoka familia ya Kikristo ya dhehebu la Coptic, anaweza
kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo iwapo atalipa dola 167 kama dhamana.
Kesi hii inazua maswala nyeti kuhusu uhuru wa
maoni wakati raia wa Misri wakijiandaa kupiga kura ya maoni
kuhusu katiba rasimu.
Wito Kutaka aachiliwe
Wanaharakati wa haki za banadamu wametoa wito kuwa Bwana Saber achiwe huru.
Kumekuwa na kesi kadhaa zinazohusiana kukufuru
baadhi ya mambo nchini Misri katika miaka miwili tangu Hosni Mubarak apinduliwe, huku wengi
wa washtakiwa ni wa dhehebu la Copts, ambao ni asilimia 10 ya idadi ya
watu nchini humo
Ingawaje kumkufuru Mungu limekuwa kosa la jinai
kwa miaka mingi, Kifungu 44 cha katiba rasimu kina kifungu maalum
kinachopiga marufu kashfa dhidi ya manabii.
Chanzo: BBC